Ujerumani yatangaza kuongeza muda bila kuiuzia silaha Saudia

Mamlaka nchini Ujerumani imtangaza kuongeza muda bila ya kuiuzia silaha serikali ya kifalme ya Saudia

1383612
Ujerumani yatangaza kuongeza muda bila kuiuzia silaha Saudia


Mamlaka nchini Ujerumani imtangaza kuongeza muda bila ya kuiuzia silaha serikali ya kifalme ya Saudia.

Mamlaka nchini Ujerumani imetangaza kuwa imechukuwa uamuzi wa kuongeza muda  bila ya kuiuzia silaha Saudia.

Uamuzi hio umefahamisha kuwa ni muda wa miezi 9 ndio ulioongezwa ambapo Ujerumani haitoiuzia silaha Saudia.

Baada ya miezi 9 huenda Ujerumani ndipo itakapoanza upya kufanya biashara ya silaha na Saudia.

Shirika la habari la Ujerumani la DPA limefahamisha  kwa kumnukuu msemaji wa  serikali ya Bi Angela Merkel  amechukuwa uamuzi wa kurefusha muda wake ambao ulikuwa umtengwa kwa ajili ya kuendelea biashara ya silaha na Saudia.

Muda huo umetangazwa  kuongezwa kwa miezi 9 hadi ifikapo Disemba  31.

Uamuzi wa kusitisha kuiuzia silaha Saudia ulichukuliwa Novemba mwaka  2018 kufuatia mauaji ya mwanahabri  wa Saudia Jamal Khashogi   katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul.Habari Zinazohusiana