Coronavirus : Idadi  ya watu waliofariki  Italia yafikia watu 6077

Idadi ya watu waliofariki kwa virusi vya corona  nchini Italia yaongezeka na kufikia watu 6077

Coronavirus : Idadi  ya watu waliofariki  Italia yafikia watu 6077


Idadi ya watu waliofariki kwa virusi vya corona  nchini Italia yaongezeka na kufikia watu 6077.

Kila kukicha nchini Italia ni majozi,  idadi ya watu  ambao wamekwishafariki  kutokana na virusi vya corona inazidi kuongezeka.

Ni watu  6077 ambao wameripotiwa  kufariki kwa virusi vya corona, watu  601 wamefariki kwa  muda wa masaa  24 na kufanya idadi hiyo kuongezeka.

Nchini Uhispania watu  2182 wameripotiwa kufariki baada ya watu  462 kufariki kwa muda wa siku moja. 

Mji ulioathirika kwa kiasi kikubwa na virusi hivyo ni jiji la Madrid.

Ufaransa kwa upande wake  idadi ya watu waliofariki  imeripotiwa kuwa watu  860 huku kesi za  watu waliokwisha ambukiwa ikifahamishwa kuwa 20000.

Idadi kubwa ya watu waliofariki imetokea Jumatatu.

Nchini Uholanzi watu 213 wamefariki huku wengine  4749 wakiwa  wameambukiwa na virusi Covid-19.

Sheria nchini Uholanzi inamkata faini yeyote yule atakae  kwenda kinyume na sheria baada ya kutangazwa kuheshimu kutokaribiana kwa mita moja na nusu.
Faini hiyo ni kuanzia Euro  400 hadi Euro 4000 kwa yeyote atakae kiukwa sheria.
 Habari Zinazohusiana