Njia tatu zinaweza kupeekea Pandemia kumalizika

Njia kuu 3 zitapelekea kumalizika kwa virusi vya Corona viivyosababisha Pandemia

1383585
Njia tatu zinaweza kupeekea Pandemia kumalizika

Imearifiwa kwamba virusi vipya vya Corona (Covid-19) vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu  vitaweza kudhibitiwa na kumalizwa kabisa kwa njia kuu tatu.

Prof. Dr. Mehmet Ceyhan, mkuu wa idara ya magonjwa ya kuambukiza kwa watoto katika chuo kikuu cha sayansi ya tiba  cha Hacettepe mjini Ankara amesema,

Katika muda wa utamio wa virusi vya Covid-19, kipindi ambacho wagonjwa hawaonyeshi dalili yeyote, ugonjwa huweza kuambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine

Ceyhan alisema,

"Muda wa utamio wa ugonjwa unatofautiana kati ya siku 2 hadi siku 14. Virusi hivi  kama ilivyo kwa mafua, menenjit, pneuomonia, sarampion na rubeola huambukizwa kwa njia ya hewa. SARS na MERS huambukiza mara baada ya kuanza kuonyesha dalili lakini Covid-19 huambukiza katika kipindi cha utamio. Ni kwa ajili hiyo kuzingatia kanuni za usafi na kujitenga na jamii ni masuala ya muhimu sana.”

Covid-19 ukilinganisha na SARS na MERS ni ugonjwa wenye maambukizi makubwa zaidi na unaweza kuzibitiwa kwa njia 3, alisema Ceyhan

“Njia ya kwanza ni wengi wa watu kujenga kinga imara na hivyo kuzuia virusi visienee zaidi njia ya pili ni kwa kupatikana kwa chanjo ya virusi hivi, njia ya tatu ni kwa virusi hivi kupata mabadiliko ambayo yatawezesha virusi hivi vishindwe kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Pandemia litamalizika  kwa moja ya njia hizo tatu., mfano ni kwa SARS ambako inazaniwa kwamba virusi alipata mabadiliko na kupoteza baadhi ya sifa. Na kwa hivyo kupelekea ugonjwa kumalizka.Habari Zinazohusiana