Corona na Mustakabali ujao wa mfumo wa kimataifa

Mifumo ya dunia inaonekana kutingishwa vibaya na virusi vipya vya Corona (Covid-19) vilivyoanzia  katika jimbo la Wuhan nchini China na kuenea duniani kote

1383155
Corona na Mustakabali ujao wa mfumo wa kimataifa

Mifumo ya dunia inaonekana kutingishwa vibaya na virusi vipya vya Corona (Covid-19) vilivyoanzia  katika jimbo la Wuhan nchini China na kuenea duniani kote. Imekuwa ni ajenda kuu ya kidunia katika miaka 10 ya hivi karibuni.

Matukio ya Septemba 11 yaliitikisa mifumo ya dunia na kusababisha changamoto ya kiulinzi, Baadae ikaja Daesh ambayo ikazidi kuongeza changamoto za kiusalama kidunia.

Mwaka 2008 dunia nzima ilikumbwa na changamoto ya kiuchumi Pamoja na kuwepo kwa tofauti ya miaka 10 inaonekana dunia inazidi kuelekea kubaya, viashiria vya kiuchumi vimeanza kugeuka kinyume nyume tena.

Wakati vita vya kibiashara vya  hivi karibuni baina ya Marekani na China vikitishia uchumi kwa ngazi ya kidunia, kuna viashiria vingine vinavyoonyesha kwamba changamoto ya kiuchumi ya kidunia inaweza kutokea.

Changamoto za kisiasa zinazojiri duniani,Kuongezeka kwa siasa kali za mrengo wa kulia, Mashirika ya kimataifa kupoteza uwezo wake wa kazi pamoja na mgogoro wa Syria ni katika masula yanayotia mashaka kwenye mustakabali wa mifumo ya kidunia.

Lakini hakuna yeyote anayefikiria kwamba changamoto hizi zitapelekea  mustakabali mbaya kwa mifumo ya dunia.Lakini mlipuko wa Corona , inavyoonekana utaiweka dunia katika mustakabali mbaya zaidi ya inavyotegemewa na mifumo ya kidunia kila uchwao inazidi kuyumba.

SETA /  Mwl. Dkt. Mkurugenzi wa utafiti wa masuala ya kiusalama Murat Yeşiltaş  anaelezea kuhusiana na mada hii...

Corona ni suala la kidunia linaloathiri usalama wa binadamu moja kwa moja.

Kuanzia miaka ya 1980 usalama wa binadamu umekuwa ni moja ya mada muhimu  katika siasa za kidunia.

Mlipuko wa Corona umeanza kuonyesha athari katika upande wa afya usalama wa binadamu na afya ya jamii katika ngazi ya kidunia.

Athari ya kwanza na muhimu bila shaka inaonekana kwenye uchumi.

Ugonjwa huu utaenda mpaka wapi na wakati gani utaweza kudhibitiwa, ni masuala ambayo kwa upnde wa afya ya binadamu yanaathiri uchumi, hasara itakayosababishwa katika afya ya binadamu na kama itaweza kurekebishwa nia masuala yanaoacha maswali.

Maswali haya yanaonekana kusababisha msikitiko katika uchumi wa kidunia.

 

Kiwango cha ukuaji wa uchumi wa China kimeonekana kuporomoka. Uzalishaji nchini China katika baadhi ya maeneo umesimama kabisa. Uchumi wa mataifa ya Italia, Ufaransa, Ujerumani na Uhispania ambao kwa kiasi kikubwa hutegemea usafirishaji nao umefikia hatua umesimama, kutokana na virusi vya Corona wadau wakubwa wa uchumi wa ulimwengu, Marekani nao wameanza kuathirika, pamoja na benki kuu ya taifa hilo kutoa kiasi cha dola bilioni 700 kusaidia uchumi usiyumbe, Pesa hizo hazijasaidia sana hali ya soko.

Mmoja wa wshauri wakuu wa shirika la IMF, Kennet Rogoff alisema uchumi wa dunia utaporomoka kufikia hatua mbaya. Taasisi ya utafiti ya Oxford ilifahamisha, nchi zinazoendelea zenye madeni ya nje zinzweza kushindwa kulipa madeni yao.

Kwa upande mwingine benki kuu ya Marekani inaweza kutumia njia ambayo  haijaitumia sana katika kuongeza ujazo wa fedha. Ufaransa kwa upande wake imetangaza itatenga bajeti kubwa ya Euro milioni 500 katika kupambana na Corona.

Pamoja na hatua hizo zinazochukuliwa  bado mdororo wa uchumi haujapungua, ni kwa sababu soko halisi linaelekea limefikia katika hali ya kusimama. Kama hali itaendelea hivi basi miaka miwili ijayo haitawezekana uchumi kurudi katika hali yake ya kawaida. Hali hii inaweza ikapelekea kudorora kwa uchumi dunnia nzima na kuanguka kwa uchumi wa mataifa yenye uchumi dhaifu.

Ni kwa ajili hiyo Virusi vya Corona zaidi ya kuyumbisha uchumi inaweza kusababisha mdororo wa kihistoria katika uchumi wa ulimwengu.

 

Upande mwingine wa mifumo ya kidunia utakaoathiriwa na Corona ni usalama wa kiulimwengu. Kama vile ilivyopata kusemwa na serikali ya jamuhuri ya Uturuki “ Tatizo ni la kidunia lakini vita ni ya kitaifa”. Hii inaonyesha mataifa yote kwanza yanajaribu kujiokoa yenyewe.

Kila taifa mwisho wa siku linapambana kujiokoa na kuokoa watu wake. Mataifa mengi kama vile China, Itaia, Ufaransa, Marekani, Uhispania na Ulaya yameanza kuchukua hatua kali kupambana na mlipuko huo.

Uturuki ni miongoni mwa mataifa ambayo tangu mwanzo yamechukua hatua kali na madhubuti.Karibu safari zote za kimataifa zipo mbioni kufungwa.

Ufaransa imetangaza kufunga karibu mipaka yote ya ardhini. Uingereza kwa upande wake inaonekana kutumia mbinu tofauti ukilinganisha na Uingereza na Ulaya.

Lakini habari zinazotufikia ni kwamba kila siku hali ya tafrani imezidi kuenea nchini humo.

Kwa upande mwingine Ufaransa imehairisha mzunguko wa pili wa uchaguzi wa serikali za mitaa; Nchini uhispania uratibu wa Hospitali binafsi umehamishiwa serikalini.

Nchini Uholanzi kwa mara ya kwnza tangu mwaka 1973 wakati wa mgogoro wa mafuta waziri mkuu wa taifa hilo ahutubia taifa.

Nchini Marekani katika maeneo ambayo ugonjwa umesambaa zaidi watu wamezidi kujimilikisha silaha.

Hali ikiendelea hivyo itasababisha kuenea kwa tafrani na kuondoka kwa utulivu miongoni mwa wanajamii na mataifa.

Mlipuko wa Corona kwa kiasi kikubwa umetingisha uchumi wa dunia pamoja na usalama wa kidunia.

Mifumo hii miwili ya kidunia, mustakabali wake utakuwaje ni suala ambalo pia linaweza kuathirika. Yatakayojiri baada ya hapo yatapelekea mataifa na wadau wote kupitia katika mchakato wa upinzani.

Hali ya kwanza ya kiupinzani  ni katika ngazi binafsi itatokea katika ngazi ya uchumi wa kitaifa.

Hatua zitakazochukuliwa na mataifa makubwa katika kupambana na virusi hazitasababisha matatizo ya kifedha, lakini mawimbi yatakayotokea katika uchumi wa kidumia yataathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa mataifa hayo.

Kwa mataifa yenye uchumi dhaifu hayatakuwa na vingi vya kupoteza.

Upinzani wa pili utaonekana katika ngazi binafsi na ya jamii,Kadiri watengeneza tafrani watakavyoongezeka ndivyo saikolojia ya tafrani katika jamii itakavyozidi, kitu ambacho kinaweza kupelekea vurugu katika jamii na hata kuanguka kwa serikali.

Ni kwa sababu hiyo upinzani wa kijamii utaathiri kwa kiasi kidogo mataifa yenye nguvu, huku athari kubwa zinatarajiwa kuonekana kwa mataifa dhaifu.

Jaribio la tatu ni katika upinzaniwa kitaifa. Katika mataifa yanayojiongoza kitaasisi na yenye nguvu, mchakato hautakuwa na athari kubwa kama  katika mataifa dhaifu. Labda inaweza kupelekea yakawa mataifa yaliyoshindwa.

Ni yumkini kwamba mara baada ya mipuko huu zitabaki athari nyingi.

Tutaona ni jinsi gani athati hizi zinaweza kutumika kama msingi wa kujenga na kuanzisha ustaarabu mpya.Habari Zinazohusiana