Mbinu za vita dhidi ya Virusi vya Corona katika mataifa 3, China, Singapur na Korea kusini

Mbinu za vita dhidi ya virusi vya Corona zilizotumika katika mataifa 3 tofauti na kuonyesha mafanikio

1382821
Mbinu za vita dhidi ya Virusi vya Corona katika mataifa 3, China, Singapur na Korea kusini

Huku China ikitumia mbinu ya kuwatenga kiufasaha walioambukizwa virusi vya Corona (covid-19), Mbinu inayotumiwa Singapur ni njia za utambuzi wa ugonjwa mapema,  Korea kusini wao wanatumia mbinu ya kupima watu wengi.

Katika kupambana na virusi vya Corona kuanzia katikati ya mwezi Januari na kuendelea mamlaka nchini China ilianza kuitenga na kuiweka katika karantini miji 16 ukiwemo Wuhan ambako ugonjwa  ndiko ulikoanzia.

Katika jimbo njia zote za usafiri ikiwemo anga na ardhini, watu walizuiliwa kutoka nje. Watu waliruhusiwa kutoka kwenda kutafuta chakula na vifaa tiba pekee. Mara baada ya kupita kipindi cha miezi miwili visa vipya vya maambukizi vilipungua kutoka maefu kwa siku kufikia makumi kwa siku. Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa liliipongeza mamlaka nchini China kwa mafanikio hayo.

Kwa upande wa Singapur mbinu yake ya kufanya utambuzi wa mapema umesaidia sana.

Jumala ya watu wenye maambukizi nchini humo imefikia 313, lakini watu hao unaweza kusema wanaishi maisha yao kawaida.

Mbinu iliyotumiwa na Korea kusini yenye idadi ya watu wapatao milioni 50 ni tofauti sana ukiinganisha na China. Siri ya mafaninikio ya nchi hii katika kuwedha kuudhibiti ugonjwa huo ipo katika kuwafanyia vipimo vya kutambua Covid-19 watu wengi zaidi.

Nchini humo zaidi ya watu 270 elfu walifanyiwa vipimo vya Covid-19 .

Inafahamika kwamba wagonjwa wenye hatari kubwa zaidi kama (wazee, wenye shinikizo la damu, kisukari, magonjwa sugu ya mapafu na moyo, wanaopatiwa tiba ya saratani) hutakiwa kulazwa hospitali. Wagonjwa wenye dalili za katikati huwekwa katika vituo maalumu vilivyotengwa  nje ya hospitali na kupewa tiba muawana. Kwa wagonjwa waliopata nafuu na kufanyiwa vipimo mara 2 na kukutwa bila virusi huruhusiwa kutoka chini ya uangalizi.

Korea kusini imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia vifo kutokana na ugonjwa huu ambapo mpaka sasa ni wagonjwa 75 pekee wamefariki kwa ugonjwa huo.Habari Zinazohusiana