Ni marufuku kuswali au kuonekana katika Misikiti mikuu ya Makka na Madina

Kujfuatia kutambuliwa kwa visa takribani mia tatu vya Corona nchini Saudia, mfame wa nchi hiyo amepiga marufuku kuswali swala za pamoja katika misikiti yote ya maka na Madina ikiwa ni pamoja na Masjid l haram na msikiti wa Mtume

1381703
Ni marufuku kuswali au kuonekana katika Misikiti mikuu ya Makka na Madina

Kufuatia visa vya virusi vya Corona kufikia takribani 300, katika taarifa iliyotolewa na mfalme wa Saudia, Mfalme Salman alisema

“ Tunaingia katika kipindi kigumu zaidia katika vita dhidi ya ugonjwa wa Corona, vipindi vifuatavyo vitakuwa vigumu zaidi.” Mwanzoni ilitolewa marufuku kuswali swala za jamaa (pamoja) katika misikiti yote ya Macca na Madina isipokuwa, msikiti mkuu wa Macca ( Masjidi l Haram) na msikiti wa Mtume Madina.

Hivi sasa marufuku imepanuliwa ambapo hata misikiti hiyo mikuu ya Macca na Madina hairuhusiwa kufanya ibada za pamoja.

Na marufuku sio tu katika kuswali bali hata kuonekana maeneo hayo.


 Habari Zinazohusiana