Azerbaijan kununua silaha za kisasa kutoka Uturuki

Waziri wa ulinzi wa Azerbaijan, generali Zakir Hasanov amesema nchi yake itaendelea kununua silaha za kisasa kutoka Uturuki

1378255
Azerbaijan kununua silaha za kisasa kutoka Uturuki

Waziri wa ulinzi wa Azerbaijan, generali Zakir Hasanov amesema wataendelea kununua silaha za kisasa, na vifaavya ulinzi kutoka Uturuki.

Kwa mujibu wa taarifa ya maandishi iliyotolewa na wizara ya ulinzi wa Azerbaijan, generali Hasanov, maafisa wa wizara, maafisa wa jeshi, viongozi wa jeshi lililopo mpakani baina ya  Armenia na Azerbaijan walifanya mkutano kwa njia ya “video conference”.

Katika mkutano huo Hasanov alilisisitiza umuhimu wa kutumia majeshi yenye vifaa vya kisasa pamoja na uongozaji wa jeshi kwa mbinu za kisasa.

"Kwa kujifunza  kutokana na udhoefu wa vita wa majeshi ya Uturuki, tutaliandaa na kuliweka tayari jeshi letu, Kwa ushirikiano wa kijeshi baina ya nchi hizi mbili tunabadilishana udhoefu, Kuanzia sasa na kuendelea tutaendelea kununua silaha za kisasa kutoka Uturuki”.

 Habari Zinazohusiana