Vita vya mafuta

IMF na mashirika ya fedha ya kimataifa yanazamia kwamba mwaka 2020 uchumi wa dunia unaweza kuanguka kutokana na janga la virusi vya Corona

Vita vya mafuta

Opec plus  jina linalotumika kwa chombo maalumu kinachoundwa na mataifa wanachama wa Opec pamoja na Urusi. Chombo hichi kwa muda mrefu kimejaribu kuleta msawazo baina ya hitajio na ugavi wa mafuta pamoja na kuhakikisha kwamba bei ya mafuta haitetereki. Maalumu, pale wazalishaji wa mafuta ya kwenye miamba wa Marekani  kadiri walipokuwa wakiongeza uzalishaji nchi wanachama wa Opec plus wamekuwa wakipoteza soko na umadhubuti wa bei, lakini pamoja na changamoto hiyo nchi za Opec plus ziliweza kuendeleza ushirikiano . Mambo yamekuwa tofauti mara baada ya mlipuko wa virusi vya Corona na haswa  virusi hivyo vilivyoanza kuenea na kuathiri mataifa mengi, uchumi wa ulimwengu umeyumba, soko la mafuta nalo limepata mtikisiko, wakati uchumi wa ulimwengu ukiyumbishwa na kupelekea mchakato mpya wa anguko kuanza, ushirikiano miongni mwa wanachama wa opec plus umeingia dosari na mataifa hayo yakaingia katika vita kamili ya mashindano ya mieleka  yakiongozwa na Saudia na Urusi.

 

SETA / Mtafiti wa siasa za kimataifa  Can ACUN   anafafanua mada hii kama ifuatavyo...

 

Virusi vya Corona vilivyoanzia katika jimbo la Wuhan nchini China na kuenea dunia nzima vimesababisha tishio dhidi ya afya ulimwenguni, pamoja na hilo vimeanza kusababisha uchumi wa dunia uyumbe kwa kiasi kikubwa. Mara  baada ya virusi hivi kushambulia haswa China na mataifa mengine yaliyoendelea huku ikishuhudiwa uzalishaji ukipungua kwa kasi, matumizi kwa watu waliowekwa karantini nayo yameanza kupungua. Kutokana na hilo, kiuhalisia mahitaji ya mafuta na bidhaa nyingine nayo yameanza kupungua. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na IMF pamoja na Benki na mashirika mengine ya fedha ya kimataifa uwezekano wa kutokea kwa anguko la kidunia ni mkubwa. Katika hali hiyo inatazamiwa kwamba kwa mwaka wote wa 2020 mahitaji ya mafuta yatapungua kwa kiasi kikubwa. Shirika la nishati duniani linatazamia kwamba   mahitaji ya mafuta yatapungua kwa mapipa milioni 3-4 kwa siku. Wakati katika soko la mafuta mahitaji yanatarajiwa kushuka kwa kiasi kikubwa, wazalishaji wa mafuta ya kwenye miamba wa Marekani wanaendelea kuongeza uzalishaji. Marekani imeanza kuzalisha kati ya pipa milioni 12 hadi 13 kwa siku. Kutokana na maendeleo ya teknolojia inayohusiana na uzalishaji wa mafuta na gesi za kwenye miamba, gharama za uzalishaji wa mafuta hayo zinapungua kila siku. Kwa wazalishaji wa kiasili wa mafuta  wanaotegemea athari za mahitaji na ugavi haswa haswa Urusi na Saudia wanakutana na changamoto kubwa za kiushindani.

Saudia inataka makubaliano ya Opec plus yaendelee ikiwezekana hata uzalishaji ushushwe kufikai mapipa milioni 1.5. Kwa upande wa Urusi wanachukulia kupunguza uzalishaji kutafaidisha mataifa washindani kama Marekani na hivyo kupelekea wao kupoteza sehemu yao ya soko kadiri siku zinavyozidi kwenda, kwa kuliona hilo Urusi haikutaka kusaini  mkataba mpya. Mkutano wa Opec uliofanyika Viyena ulimalizika bila mafanikio, na hatimaye wanachama wakaanza kutishiana misuli. Urusi na na Sudia zote zimetangaza kuongeza uzlishaji wa mafuta. Katika hali hii inatazamiwa bei ya mafuta itapungua kwa asilimia 30. Kwa mujibu wa wataalamu wa sekta husika wanasema bei ya mafuta inaweza kushuka kufikia dola 20 kwa pipa. Bei itasababisha mtikisiko mkubwa wa uchumi katika nchi zinazozalisha mafuta.

 


Tagi: Saudia , Urusi , Opec

Habari Zinazohusiana