Oparesheni Ngao ya Chemchem

Kufuatia kuuawa kwa askari jeshi 33 wa Uturuki huko Idlib, Uturuki katika kujibu mapigo imeanzisha oparesheni kubwa ya kijeshi ambayo lengo lake kubwa ni kulinda mipaka kwa mujibu wa mkataba wa Sochi. Oparesheni hii imeifanya Idlib kuwa habari kuu duniani

1372438
Oparesheni Ngao ya Chemchem

Katika wiki za hivi karibuni imeonekana kwamba mapigano yanayoendelea Idlib, yamechukua sura mpya. Mashambulizi makali ya ardhini na angani yanayofanywa na vikosi vya utawala wa Assad kwa kusaidiwa na Urusi katika kufanikisha  kuzikamata barabara kuu M4 na M5 ambazo zina umuhimu mkubwa wa kimkakati, na upinzani unaotolewa na vikosi vya Uturuki umefanya Idlib iingie katika habari kubwa zaidi duniani.  Mnamo Februari 27 vikosi vya Assad vilifanya shambulizi la hila dhidi ya majeshi ya Uturuki na kusababisha vifo vya askari jeshi 33 wa Uturuki, tukio hilo lilisababisha mgogoro wa Idlib uzidi kuwa mkubwa na kuilazimisha Uturuki kutoa majibu makali zaidi kwa utawala. Kutokana na kwamba haikufahamika kama Urusi ilihusika na shambulizi la anga dhidi ya vikosi vya Uturuki, Ankara moja kwa moja ikachukulia kwamba mashambulizi yale yalifanywa na vikosi vya utawala. Jeshi la Uturuki likapeleka hasara kubwa kwa vikosi vya utawala Idlib. Pamoja  na kwamba hali hii imepelekea kwa mara ya  kwanza katikahistoria ya vita vya Syria mataifa mawili kukabiliana vikali, oparesheni za Uturuki zimepelekea wadau wote katika mgogoro wa  Syria kutazama kwa umakini nafasi zao.

 

 

SETA /  Mkurugenzi wa tafiti za Ulinzi, Mwandishi. Mwl. Dkt. Murat Yeşiltaş anafafanua kuhusiana na mada hii...

 

Uturuki imetangaza kuanza kutekeleza oparesheni kubwa ya kijeshi ambayo imepewa jina “ Bahar Kalkanı” ikimaanisha ngao ya chemchem. Katika historia ya vita vya ndani vya Syria haijawahi kutokea Uturuki na Syria zikakabiliana namna hii. Pomaja na kuwa Uturuki imezitawanya ndege zake za kivita katika anga lake pia  kwa kutumia ndege zenye silaha zisizobeba binadamu “drones”, huingia katika anga la Syria nakushambulia maeneo muhimu ya vikosi vya utawala.Katika siku ya pili ya mapambano askari na wanamgambo zaidi ya  2500 (takwimu rasmi) wa vikosi vya utawala wa Assad na washirika wake waliangamizwa. Pamoja na hayo takribani vifaru vya vita 100 na ndege za kivita aina ya SU 24na L 36 ziliharibiwa. Hasara kwa utawala wa Assad haikuishia hapo mifumo ya ulinzi wa anga,  mizinga ya kurushia makombora na vyombo vingine vingi vya kivita ni katika hasara iliyopata utawala wa Assad, kutokana na kuharibiwa na mashambulizi ya Uturuki. Hivyo Uturuki iliamua kujibu mapigao sio tu kwa kushambulia askari bali kwa kuwa na mkakati wa kusababisha hasara kubwa kwa utawala kadiri iwezekanavyo. Kwa kutumia ndege zisizoongozwa na rubani katika kufanya mashambulizi, Ankara imeweza kuonyesha uwezo wa aina yake katika historia ya medani ya vita.

Malengo ya mkakati yapo wazi, Kuvilazimisha vikosi vya utawala kuondoka ndani ya mipaka ya eneo lilitokana na makubaliano ya Sochi. Pamoja na hasara kubwa kwa upande wa anga ambayo vikosi vyaa utawala imepitia dalili zinaonyesha kwamba vikosi hivyo haviko tayari kuondoka katika maeneo waliyopo. Hili linaweza kujidhihirisha kutokana na mara kwa mara kubalika kwa udhibiti wa eneo la Serakip ambalo ni muhimu na la kimkakati katika udhibiti wa barabara kuu za kimkakati za M4 na M5. Pamoja na kwamba Moscow haikuonyesha mwenendo wowote baada ya hasara kubwa iliyosababishwa kwa jeshi la utawala katika siku ya kwanza ya oparesheni, Baadae imeonekana jinsi Moscow ilivyoonyesha sehemu yake wazi wazi. Moscow ilisambaza askari jeshi wake katika eneo la Serakib hivyo ndio kusema jeshi la Urusi limewekwa mbele ya vikosi vya Uturuki katika kuzuia uwezekano wa Uturuki kuparnua eneo la oparesheni. Hali hii inapelekea Uturuki itake au isitake kufuata mwenendo wa kuwa makini zaidi. Hata hivyo mpaka sasa hakuna mazingira ambayo yatasababisha nchi hizi mbili zipigane moja kwa moja. Ni kwa ajili hiyo Putin na Erdoğan 5 watakutana mjini Moscow, Machi 5 kujadiliana hatima ya Idlib.

 

Wakati Uturuki ikitaka mipaka iheshimiwe kulingana na mkataba halisi wa Sochi, inaonekana nia ya Moscow ni tofauti. Inaonekana pia miongoni mwa wadau hawa wawili hakuna anayetaka mgogoro huu ukue zaidi. Ni kwa ajili hiyo mkutano wa Machi 5 una umuhimu wa kipekee. Au maelewano yapatikane na mahusiano baina nchi hizi mbili yaendelee au maelewano yasipatikane na hivyo mgogoro uendelee kuwa mkubwa zaidi. Yumkini ikawezekana kufikia muafaka utakaokuwa na faidi kwa pande zote mbili, na hilo ndio litakuwa suluhisho sahihi.Habari Zinazohusiana