Ruhani: " Virusi vya Corona vimekuja kama mgeni asiye na mwaliko"

Rais Hasan Ruhani wa Iran amewataka raia wa Iran wasihamaki na wafuate maelekezo yatayotolewa na wizara ya afya

1366363
Ruhani: " Virusi vya Corona vimekuja kama mgeni asiye na mwaliko"

Hasan Ruhani Rais wa Iran amefananisha ugonjwa unaotokana na virusi vipya vya Corona (Kovid-19) ambao umesababisha vifo vya watu wengi nchini kwake na “mgeni asiye na mwaliko”,

Ruhani alitoa taarifa kuhusiana na virusi vya Corona wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa barabara kubwa inayounganisha Tehrani na kusini mwa nchi.

Ruhani amewataka watu wasizame katika uoga na wafuate maelekezo yatakayotolewa na wizara ya afya.

“ Corona sio hatari zaidi ya virusi vya influenza B, sisi tunakinga dhidi ya virusi hivyo, na Corona pia tutaipatia chanjo. Virusi vya Corona ni kama vile mgeni aliyekuja bila ya mwaliko  na ameenea katika mataifa yote”.Habari Zinazohusiana