Uhusiano baina ya Uturuki na Urusi unapitia wakati mgumu

Mgogoro wa Idlib unayaweka mahusiano baina ya Uturuki na Urusi katika mtihani mkubwa

1363136
Uhusiano baina ya Uturuki na Urusi unapitia wakati mgumu

Kihistoria uhusiano baina ya Uturuki na Urusi umekuwa wenye kupanda na kushuka. Katika miaka ya vita baridi uhusiano baina ya mataifa haya mawili, hauwezi kusemwa ulikuwa mzuri sana. Kutokana na uhusiano baina ya Uturuki na Marekani kuzorota mwaka 1964 kwa Marekani kuiwekea vikwazo vya silaha Uturuki, Uturuki ilijaribu kufuata sera za kujisogeza karibu kwa Urusi, lakini haikufanikiwa sana. Baada ya kumalizika kwa vita baridi na kuparaganyika kwa Muungano wa Kisovieti ikapatikana nafasi kwa mara nyingine ya kuweza kurekebisha mahusiano baina ya Ankara na Moscow, hilo halikufanyika kutokna na utafauti wa mataifa haya kuhusiana na eneo la Balkan, bahari Nyeusi na Caucasia. Hivi sasa katika utaratibu mpya wa dunia mataifa hayo yamejikuta katika kutafuta madaraka mapya,  ni kwa ajili hiyo pia mahusiano hayajafikia katika kiwango kinachohitajika.

SETA /  Mkurugenzi wa tafiti za masuala ya, Mwandishi.Mwl.Dkt Murat Yeşiltaş anafafanua kuhusiana na maada hii...

  

Katika miaka ya 2000 Uturuki na Urusi kwa pamoja zilifanya juhudi ya kujenga misingi imara ya ushirikiano ulion na tija. Pamoja na Moscow kuiona Ankara kama mpinzani mara kadhaa kila ilipohitajika Moscow iliichukulia Ankara kama mshirika hasa katika biashara ya nishati. Ankara nayo kwa upande wake ilichagua kufuata siasa ya kuiona Moscow kama jirani mkubwa, katika suala la gesi asilia ikaagiza kutoka Moscow na pia kushirikiana na Moscow katika utatuzi wa migogoro ya kikanda. Matokeo yake Uturuki na Urusi zikaanzisha ushirikiano katika mambo mengi, na kikawa ni kipindi cha kujenga ukaribu.

 

Mgogoro wa Syria umerudisha hali ya mataifa haya mawili kuwa mahasimu. Kwanza mnamo mwaka 2015 Uturuki iliidungua ndege moja ya kivita ya Urusi iliyovunja sheria na kuruka katika anga la Uturuki bila idhini, hilo likapelekea mgogoro mkubwa baina ya mataifa hayo. Mnamo mwaka 2016 kutokana na diplomasia baina ya pande zote kwa mara nyingine tena uhusiano ukatengemaa. Tangu hsiku hizo mpaka hivi sasa Uturuki na Urusi zimekuwa zikifuata zaidi siasa za kuwekana karibu na kudumisha uhusiano kimkakati. Lakini kutokana na msaada ambao Urusi inautoa kwa utawala Assad huko Idlib, ambako ndio ngome ya mwisho ya wapinzani, pamoja na mashambulizi ya anga ambayo yenyewe Urusi imekuwa ikiyandesha Idlib imepelekea tena uhusiano baina ya Uturuki na Urusi kuyumba.

 

Pasina shaka uhusiano baina ya Uturuki na Urusi sio tu katika mpaka wa Syria. Moscow inaishutumu Uturuki kushindwa kutekeleza matakwa ya makubaliano ya Sochi kuhusiana na Idlib. Na hivyo basi yenyewe imeamua kumaliza makundi yote yenye siasa kali katika eneo hilo.Uturuki yenyewe inajitetea kwamba ili iweze kutekeleza majukumu yake inapaswa kwanza vikosi vya majeshi ya Assad visimamishe mashambulizi. Hivyo basi kama mashambulizi hayatasimama ni vigumu kwa Uturuki kuweza kufanikiwa huko Idlib.

Hali inapelekea uhusiano baina ya Moscow na Ankara kuingia katika mgogoro kwa mara nyingine. Nchi hizi mbili zinaweza tena kuingia katika mkwamo wa mahusiano.

Serikali ya Uturuki katika kuzuia kuzorota kwa mahusiano baina ya mataifa haya mawili, imekuwa ikisisitiza juu ya faida za pamoja kwa mataifa yote mawili zinazotokana na uhusiano mwema. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja  na  Uturuki kununua mfumowa ulinzi wa anga S 400 kutoka Urusi. Pamoja na Marekan kupinga katakata Uturuki kufanya manunuzi hayo kutoka Urusi, Uturuki bado ikathamini kwa kiasi kikubwa uhusiano wake na Urusi na kufanya manunuzi hayo. Zaidi ya hapo Uturuki na Urusi zikakubaliana kushirikiana katika viwanda vya kiulinzi. Kwa upande mwingine mataifa haya mawili yanaendesha  mradi wa pamoja utakao wezesha Uturuki kukidhi mahitaji yake ya nishati ya kinyuklia. Katika mrad huu Urusi inataka pia kuonyesha uwezo wake katika nishati ya nyuklia. Ushirikiano huu katika nyanja  hizo mbili unaangaliwa kama kitu kitachoisaidia Urusi pia ambayo uchumi wake haufanyi vizuri sana. Tukija katika suala la nishati mataifa haya mawili pia yanahitajiana. Uturuki ni mmoja wa wanunuzi wa wakubwa wa gesi asilia kutokea Urusi. Kwa hali hiyo ni mteja muhimu sana lakini vilevile ili gesi asilia ya Urusi iweze kufika Ulaya, kwakupitia Uturuki ndilo suala lenye tija zaidi. Hivyo basi kuna mambo mengi yanayo yaunganisha mataifa haya. Kwa warusi wengi Uturuki imekuwa pepo yao ya utalii wa gharama nafuu. Kwa Uturuki pia ukiangalia takwimu za watalii, Urusi inaongoza kwa kushika namba moja kwa kutoa watalii wengi zaidi wanaotembelea Uturuki.

 Kuhusiana na suala la Syria, pamoja na kwamba mataifa haya mawili yameshindwa kuelewana bado ni yote ni wadau muhimu. Hata kama Urusi itatangaza ushindi wa kijeshi huko Syria lakini bila ya ushirika wa Uturuki katika misingi ya kidiplomasia itakuwa ni vigumu kufikia utulivu utakaodumu katika eneo hilo. Kuua raia zaidi na kuwahamisha wengine katika maeneo yao kuwalazimisha waelekee upande wa Uturuki, haunekani kama ni  mkakati wa kiakili sana kwa upande wa Urusi. Kwani kinyume chake hilo linaweza sababisha gharama zaidi kwa Urusi. Katika siku za hivi karibuni Marekani imeanza kuona fursa katika suala hili na imeanza kuchukua hatua za kuharibu kabisha uhusiano baina ya Uturuki na Urusi. Kubwa zaidi ni Marekani kutangaza itakuwa upande wa Uturuki katika suala la Idlib.

Kama Uturuki na Urusi hazitaweza kuweka tofauti zao pembeni, basi mvutano mpya baina ya Ankara ni Moscow utadhihirika na huo ndio utakuwa mwanzo wa juhudi zote zilizofanyika kuboresha mahusiano baina ya mataifa haya mawili kuingia dosari na kurudi nyuma. Ni kwa ajili hiyo Idlib unakuwa ni mtihani mkubwa katika mahusiano ya mataifa haya mawili, Ili Urusi iweze kudumisha uhusiano wa kimkakati na Uturuki inapaswa kuacha mara moja mahitajio yake ya kibabe huko Idlib  na vile vile kusimamisha mara moja mashambulizi yanayofanya na vikosi vya utawala.

 Habari Zinazohusiana