Jeshi la Syria linatakiwa kuacha chokochoko zake

Muakilishi wa Uturuki Umoja wa Mataifa asema kuwa jeshi la Syria linatakiwa kuondoa kambi zake karibu na jeshi la Uturuki

1363127
Jeshi la Syria linatakiwa kuacha chokochoko zake


Muakilishi wa Uturuki Umoja wa Mataifa asema kuwa jeshi la Syria linatakiwa kuondoa kambi zake karibu na jeshi la Uturuki.

Muakilishi wa Uturuki Umoja wa Mataifa  asema kwamba jeshi la Syria linatakiwa kuondoka kabla ya Februari kumalizika.

Feridun Sınıroğlu , muakilishi wa Uturuki Umoja wa Mataifa amesema kuwa jeshi la Uturuki halitosika kujibu vikali iwapo litatishiwa usalama na jeshi la Syria katika  vituo vyake vya ulinzi Idlib.

Jeshi la Syrşa linatakiw akuondoa vikosi vyake karibu na maeneo ambapo jeshi la Uturuki limetia kambi na  kuweka vituo vya ulinzi baada ya kusainiwa makubaliano ya Sochi.

Hayo  muakilishi wa  Uturuki Umoja wa Mataifa ameyazungumza katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano.

Imefahamishwa kuwa ni watu zaidi ya milioni   walilazimika kuhama makazi yoa  miezi miwili iliopita kufuatia  mashambulizi yalioendeshwa na  jeshi la Assad.Habari Zinazohusiana