Donald Trump ampongeza  rais Erdoğan kwa juhudi zake Idlib nchini Syria

Rais wa Marekani ampongeza rais Erdoğan kwa  juhudi zake Idlib nchini Syria

Donald Trump ampongeza  rais Erdoğan kwa juhudi zake Idlib nchini Syria


Rais wa Marekani ampongeza rais Erdoğan kwa  juhudi zake Idlib nchini Syria.

Donald Trump rais wa Marekani amempongeza rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan kwa juhudi zakeIdlib nchini Syria.

Rais Erdoğan amezungumza na rais Trump kwa  njia ya simu na kuzungumza kuhusu hali iliopo Idlib nchini Syria.

Msemaji wa ikulu ya White House, Judd Deere  ametoa taarifa kuhusu mazungumzo hayo kati ya rais Erdoğan na rais Trump yaliofanyika Jumamosi.

Kwa mujibu wa rais Trump , Uturuki inastahili pongezi kwa  kuzuia janga Idlib.

Rais Trump  amesema kuwa anayo matarajio  kuwa  Urusi itaacha kuiunga mkono serikali ya Syria na kuanza juhudi za   kisiasa kupatia ufumbuzi mzozo  uliodumu kwa zaidi ya miaka  mitano Syria.

Rais wa Marekani ameendelea kufahmisha kuwa  kuingilia kati mzozo wa Libya kutazidisha hali iliopo kuwa mbaya zaidi.
 


Tagi: Erdoğan , Trump , Syria

Habari Zinazohusiana