Mpango wa karne wa Trump ni tishio   katika ukanda

Rais wa Uturuki asema kuwa mpango wa amani wa karne wa rais wa Marekani ni tishio katika ukanda

Mpango wa karne wa Trump ni tishio   katika ukandaRais wa Uturuki asema kuwa mpango wa amani wa karne wa rais wa Marekani ni tishio katika ukanda.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kwamba  mpango wa amani ambao rais Trump  amesema kuwa ndio mpango wa karne Mashariki ya Kati ni tishio katika ukanda.

Tunasubiri  shirikisho la ushirikiano wa mataifa ya kiislamu kuandaa mkutano  wa wanachama wake  kwa ajili ya kuonesha  msimamo wa pamoja dhidi ya mpango huo wa rais wa Marekani amesema rais  Erdoğan.

Hayo rais  Erdoğan ameyazungumza  katika mkutano wake na wanahabari  akiwa katika ndege kutoka nchini Pakistani ambapo alikuwa katika ziara yake rasmi.

Katika mkutano wake huo na wanahabari, rais Erdoğan amesema kuwa  kunasubiriwa mkutano wa mataifa ya kiislamu kufanyika ili kuchukuliwa maamuzi ya pamoja dhidi ya mpango huo wa rais wa Marekani kuhusu Mashariki ya Kati.

Mataifa ya Afrika na Umoja wa Ulaya hayakubaliani na mpango huo,  msimamo huo  unaonesha matumaini Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wa Trump ameendelea kufahamisha rais Erdoğan.
 Habari Zinazohusiana