Idadi ya vifo na maambukizi ya virusi vya Corona yaongezeka kufikia watu 1524

Virusi vipya vya Corona vyazidi kuwa tishio nchini China huku idadi ya vifo na maambukizi kwa siku vikiongezeka mara dufu

1360015
Idadi ya vifo na maambukizi ya virusi vya Corona yaongezeka kufikia watu 1524

Idadi ya vifo vilivyosababishwa na maambukizi ya virusi vya Corona (Kovid-19)  huko nchini China imepanda hadi kufikia watu 1524.

Baraza la afya la taifa nchini China limetoa taarifa kwamba mpaka idadi ya watu wanaodhaniwa kuwa waliambukizwa na hivyo kuwekwa chini ya uangalizi ni watu  laki 1 na elfu 69 na 39.  Mpaka sasa idadi ya watu waliowekwa chini ya uangalizi imepungua kwa kesi elfu 8 na 689.

Mpaka hivi sasa idadi ya watu ambao ilithibika kwamba wameambukizwa imeongezeka kufikia watu elfu 66 na 492 miongoni mwao watu  elfu 8 na 969 hali zao za kiafya ni mbaya sana.

Nchini humo kwa ujumla idadi ya watu waliopata nafuu na kuruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu ni watu elfu 8 na 96.

Katika siku za hivi karibuni idadi ya vifo na maambukizi imetia fora kwani katika masaa 24 walifariki wagonjwa 143 na maambukizi mapya kufikia elfu 2 na 277.

 


Tagi: #Corona , #China

Habari Zinazohusiana