Seehofer aonya juu ya janga jipya la wakimbizi

Akosoa sera za Umoja wa Ulaya katika kushuhulikia wakimbizi kwa kuziita ni za kusuasua

Seehofer aonya juu ya janga jipya la wakimbizi

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Horst Seehofer, atoa onyo kwa Ujerumani nan chi nyingine za Umoja wa Ulaya kuhusiana na janga la wakimbizi linalowakabili.

Katika maelezo aliyoyatoa kupitia gazeti la Bild alisema katika nchi zinazozunguka bara la Ulaya kumekuwa na migogoro mingi inayosababisha watu kuyakimbia makazi yao, Ni kutokana na hilo kumekuwa na shinikizo kubwa la wakimbizi katika mipaka ya Ulaya.

Akifananisha  na janga la wakimbizi la mwaka 2015 Seehofer alisema,

"Kama tusipoyasaidia mataifa tunayopakana nayo kuweza kudhibiti wakimbizi, basi ya mwaka 2015 yatajirudia kwa mara ya pili”

Seehofer alikosoa sera za Umoja wa Ulaya kuhusiana na wakimbizi,

“Inabidi tulimalize hisi suala sasa hivi na tuache kusuasua”, alisema Seehofer.Habari Zinazohusiana