Kulazimisha amani kwa vikosi vya utawala wa Syria na washirika wake

Kufuatia majeshi ya utawala wa Syria na washirika wake kutafuta ushindi wa kivita katika medani, Uturuki inalazimika kujibu mapigo kulinda usalama wake

Kulazimisha amani kwa vikosi vya utawala wa Syria na washirika wake

 

Vikosi vya utawala wa Asad kwa kusaidiwa na Urusi na Iran vimeendelea kukiuka makubaliano ya Astana huko Idlib kwa kuendeleza mashambulizi. Katika kuhakikisha vinadhibiti barabara muhimu za kimkakati (M4 na M5), vikosi hivyo vya utawala vimedhibiti maeneo kuanzia Serakib hadi al Ays. Katika mwaka mmoja wa hivi karibuni takribani watu milioni 1 na nusu wamelazimika kuyahama makazi yao. Katika muktadha wa ujumla wa oparesheni za Idlib, Utawala na washirika zaidi ya kutafuta utatuzi wa kisiasa wanatafuta ushindi wa kijeshi. Hatua za kijeshi za Uturuki ni katika kuzuia hayo yasitokee.            

                                                                                 

SETA /  Mtafiti wa siasa za kimataifa Can ACUN

 

 anafafanua kuhusiana na mada hii...

Vikosi vya utawala katika wiki 2 za hivi karibuni vimezidisha mashambulizi huko Idlib huku kwa upande wa ardhini vikisaidiwa na wanamgambo wa kishia wanaohusishwa na Iran na angani wakipata msaada mkubwa kutoka kwa Urusi. Hilo limepelekea vikosi hivyo kuweza kusonga mbele dhidi ya  wapinzani. Mara baada ya kuudhibiti mji wa Maaret el Numan ambao ni mji  mkubwa zaidi Idlib vikosi hivyo vilisonga mbele kuelekea kaskazini na kufanikiwa kudhibiti pia  kijiji cha Serakib ambacho kina umuhimu wa kimkakati kwani kinaunganisha barabara mbili kuu na muhimu za M4 na M5. Mamia kwa maelfu ya watu wakajikuta chini ya mvua nzito za mabomu na silaha nyingine, watu hao wakaanza kukimbia kuelekea katika mpaka wa Uturuki. Uturuki kuona hivyo ikabidi iviimarishe vikosi vyake vilivyopo nchini Syria na kutoa upinzani kwa vikosi vya utawala. Na zaidi mara baada ya askari wa utawala kuwashambulia moja kwa moja askari jeshi wa Uturuki katika maeneo ya Serakib na Teftanaz, kwa mara ya kwanza Uturuki ikajikuta inalazimika kujibu mapigo kwa kuvilenga vikosi vya utawala kwa kiasi kikubwa.

 

Rais Erdoğan amesema kama mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Februari vikosi vyutawala havitaondoka ndani ya mipaka iliyotokana na makubaliano ya Sochi basi Uturuki itafanya oparesheni ya kijeshi kuviondoa vikosi hivyo.

 

Rais Erdoğan akizungumzia kuhusu Uturuki kuviimarisha vikosi vyake vya jeshi huko Idlib alisema, Uturuki imebadili mtindo wa oparesheni katika kanda hiyo na hivi sasa zama mpya zimeanza inavyoonekana. Uturuki bado inasisitiza na kusihi mipaka iliyotokana na makubaliano ya pande zote yaliyofanyika Sochi, Urusi iheshimiwe na kama hilo halitatokea, na kwa kiasi kikubwa inaonekana halitatokea,  Inaonekana vikosi vya utawala vimepanga mashambulizi zaidi dhidi ya majeshi ya Uturuki na vituo 12 vya uangalizi mjini Idlib. Hilo likifanyika Uturuki itafanya oparesheni ya kijeshi kujibu mapigo.

 

Hatua za utawala kwa kusaidiwa na Urusi katika siku za hivi karibuni zinatishia usalama wa Uturuki. Umefikia wakati Urusi inabidi itambue kuipa thamani Uturuki kama mshirika wake, Gharama za kuutatua mgogoro huu kwa vita zimezidi kuwa kubwa kwa Uturuki. Urusi inabidi itambue umuhimu wa amani na kulifanyia kazi suala hilo.

 Habari Zinazohusiana