Uturuki yaja na kipimo cha kutambua virusi vya Corona

Waziri wa afya wa Uturuki, Fahrettin Koca amesema wametengeneza kipimo kinachoweza kutambua virusi vya Corona kwa ufanisi wa asilimia 100 ndani ya muda mfupi zaidi kuliko vipimo vyote vilivyopo hivi sasa.

Uturuki yaja na kipimo cha kutambua virusi vya Corona

Uturuki imetengeneza kipimo cha kuweza kutambua virusi vipya vya Corona.

Katika maelezo ya waziri wa afya wa Uturuki, Fahrettin Koca, alisema  kwamba vipimo vilivyopo hivi sasa kwa ajili ya utambuzi  wa virusi vya Corona hutoa majibu katika muda wa kati ya saa 4-24. Kutokana na hilo wataalamu waliamua kufanya kazi kuweza kuja na kipimo kitakachotoa majibu mapema zaidi.

“Kipimo hicho kimekamilika wiki iliyopita. Kipimo hicho kimeweza kuupunguza muda wa kupata majibu kwa dk 90 -120. Kimeanza kutumika katika maabara yetu siku ya alhamis wiki iliyopita,ufanisi wa kipimo hicho ni karibu asilimia 100”.

Koca alieleza pia kwamba gharama ya kutengeneza kipimo hicho imepungua kwa wastani wa asilimia 25.

“Uingereza, Ufaransa na Ujerumani nao wametengeneza vipimo vinavyofanana, lakini vipimo vyao havijaweza kupunguza muda wa kupata majibu. Wataalamu wetu wanaendelea kufanya kazi kuhakikisha wanapunguza zaidi muda wa kupata majibu kutokana kwa kutumia kipimo hicho. Katika wiki zijazo muda huo utapunguzwa zaidi.”

Waziri wa afya, Fahrettin Koca alisema kwamba kipimo hicho kitauzwa pia nje ya nchi.Habari Zinazohusiana