Mkutano kati ya Uturuki na Urusi  kufanyika mjini Moscow

Mkutano kati ya tume maalumu kutoka Uturuki na Urusi kufanyika mjini Moscow

Mkutano kati ya Uturuki na Urusi  kufanyika mjini Moscow


Mkutano kati ya tume maalumu kutoka Uturuki na Urusi kufanyika mjini Moscow. 

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kwamba mkutano kati ya tume  maalumu kutoka Uturuki na Urusi unatarajiwa kufanyika mjini Moscow  katika siku za hivi karibuni.

Tume itakayoundwa na wizara ya mambo ya nje , wizara ya ulinzi na  upelelezi  za Ututuki na Urusi zitakutana mjini  Moscow na kuzungumza kuhusu sauala husika.

Mkutano huo  haujafahamishwa lini utafanyika.

Rais wa Uturuki amezungumza kwa njia ya simu na rais wa Urusi Vladimir Putin na kuafikiana kuhusu mkutano mjini Moscow katika siku  chache zijazo.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wawili wamejadili kuhusu hali inayoendelea Idlib nchini Syria baada ya wanajeshi wa Uturuki kushambuliwa na jeshi la Assad.

Akiongea na wanahabari, rais Erdoğan amewafahamisha kuhusu mazungumzo yake na  rais wa Urusi.
 Habari Zinazohusiana