Canada yawaondoa raia wake 188 waliokuwa Hubey nchini China

Wizara ya mambo ya nje ya Canada imetangaza kuwaondoa raia wake 188 waliokuwa Hubey nchini China

Canada yawaondoa raia wake 188 waliokuwa Hubey nchini China


Wizara ya mambo ya nje ya Canada imetangaza kuwaondoa raia wake 188 waliokuwa Hubey nchini China .

Waziri wa mambo ya nje wa Canada  François-Philippe Champagne amesema kuwa raia 188 wa Canada waliokuwa katika jimbo la Hubey nchini China  wamesafirishwa kutoka nchini humo kufuatia janga la virusi vya corona vilivyoikumba China tangu mwishoni mwa mwaka  2019.

Watu zaidi ya  1100 wamekwishafariki kutokana na virusi  vya corona  aina ya "Covid-19".

Wizara ya mambo ya nje kwa ushirikiano na wizara ya afya nchini Canada vimefahamisha kuwa watu hoa 188 wamepelekwa katika kituo cha afya ambapa watafanyiwa uchunguzi  kwa muda wa  siku kadhaa.

Kituo hicho cha afya  kinamilikiwa na jeshi katika mji wa Trenton  Ontario.

Watu wengine 213  waliosafirishwa kutoka Wuhan , uchunguzi wa kiafya  utaendelea kwa zaidi ya wiki mbili.

Nchini Canada, ni watu 7 ambao wamepimwa na kukutwa na virusi vya corona.
 Habari Zinazohusiana