Mwanamfalme Charles wa Uingereza aunga mkono juhudi za kudai uhuru za wapalestina

Asema matamanio yake makubwa ni kuona mustakabali unaleta uhuru, haki na usawa kwa raia wote wa Palestina ili wote waishi kwa ufahari na ustawi

Mwanamfalme Charles wa Uingereza aunga mkono juhudi za kudai uhuru za wapalestina

Mwanamfalme Charles wa Uingereza amesema anatamani kuona raia wa Palestina wakifaidika na uhuru, haki na usawa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na shirika rasmi la habari la Palestina, WAFA imesema Prince huyo alikutana na viongozi wa Palestina na viongozi wa dini za kiislamu na kikristo katika mji wa Palestina wa Bethlehemu.

Katika mkutano huo Prince Charles alisema anaunga mkono dua zinazofanywa kila siku kuombea amani ya kudumu. 

"Suala hili inabidi tulifuatilie kiimani na inabidi tuoneshe juhudi za kuyaponya majeraha yaliyo sababishwa na maumivu kama haya. Matamanio yangu makubwa ni kuona mustakabali unawaletea wapalestina wote usawa, haki na uhuru na kuwaona wakiishi kifahari na ustawi mkubwa. Hakuna yeyote anayefanya ziara Bethlehmu anaweza kudharau dhiki na hali ya hapa”.

 Habari Zinazohusiana