Mkono wa pole  kwa uturuki kutoka katika mataifa tofauti

Uturuki yapokea   ujumbe wa pole kutoka katika mataifa tofauti ulimwenguni baada ya tetemeko la ardhi

Mkono wa pole  kwa uturuki kutoka katika mataifa tofauti


Uturuki yapokea   ujumbe wa pole kutoka katika mataifa tofauti ulimwenguni baada ya tetemeko la ardhi.

Uturuki imetpokea mkono wa pole kutoka katika mataifa tofauti ulimwenguni baada ya  eneo lake la Mashariki kukumbwa  na tetemeko la ardhi.

Tetemeko la ardhi ambalo lilikuwa na ukubwa wa  6,8 katika kipimo cha Richter limetokea mkoani Elazığ na kusikika katika maeneo jiraji  limesababisha vifo vya watu  22 na kuwajeruhi wengine zaidi ya  1000. 

Tetemeko hilo limetokea majira ya usiku Jumaa muda mchache baada ua ibada ya usiku.

Ujumbe kutoka katika mataifa tofauti umewatakia afya njema wahanga wa tetemeko hilo .

Mustafa Akıncı rais wa Jamhuri ya Uturuki ya Kupro Kaskazini ameatakia afya njema  wahanga wa tetemeko hilo, waziri mkuu wa Ugiiriki Kyriakaos Mitsotakis  ameandika katika ukurasa wake wa Twitter akifahamisha kuwa karibu na waturuki baada  ya tetemeko hilo ambalo limesababisha maafa na uharibifu.

Waziri wa mambo ya nje Ugiriki amempigia simu waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuioğlu na kumpa mkono a pole.

Rais wa Kosovo Hashim Thacı  ameandika pia katika ukurasa wake wa Twitter  akisema Kosovo ipo pamoja na waturuki katika kipindi hiki cha majonzi.

Tume ya Umoja wa Ulaya ametoa pia mkono wa pole kwa Uturuki.
 Habari Zinazohusiana