Malkia Elizabeth wa Pili akubali Uingereza kuondoka Umoja wa Ulaya

Malkia Elizabeti wa Pili akubali Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya Januari 31

Malkia Elizabeth wa Pili akubali Uingereza kuondoka Umoja wa Ulaya


Malkia Elizabeti wa Pili akubali Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya Januari 31.
Elisabeth wa Pili, malkia wa Uingereza  akubali Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya ifikapo Januari 31 mwaka  2020.

Taarifa iliotolewa  na shirika lla habari la Uingereza BBC imesema kuwa  nyaraka zilizofanyiwa marekebesho ambazo zinalengo Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya "Brexit"  zitapitishwa kuwa sheria  nchini Uingereza.

Brexit ilikuwa ajenda ya Umoja wa Ulaya tangu miaka mitatu na nusu iliopita baada ya Uingereza  kupiga kura mwaka 2016 kutaka kuondoka Umoja wa Ulaya.

Januari 31 mwaka  2020 Uingereza itaondoka katika Umoja wa Ulaya  baada ya kuchaguliwa Boris Johnson  kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza  Disemba   mwaka  2019.

Uingereza ndio itakuwa taifa la kwanza kuondoka Umoja wa Ulaya tangu kuundwa  kwake  mwaka  1993.

Licha ya kuondoka kwake katika Umoja  huo mazungumzo kuhusu  ushirikiano wa kibiashara yataendelea.
 Habari Zinazohusiana