Idadi ya watu waliofariki katika shambulizi Idlib yaongozeka

Idadi ya watu waliouawa katika shambulizi la jeshi la Urusi Syria yongezeka

Idadi ya watu waliofariki katika shambulizi Idlib yaongozeka


Idadi ya watu waliouawa katika shambulizi la jeshi la Urusi Syria yongezeka .

Idadi ya watu waliofariki katika  shambulizi la anga la jeshi la Urusi Idlib yaripotiwa kuongezeka na  kufikia watu 26.

Idadi ya raia waliouawa imeongezeka kutokana na majeraha waliokuwa nayo.

Upinzani nchini Syria kupitia mitandoa ya kijamii umefahamisha kuwa ndege za kivita za jeshi la Urusi  zilishambulia  Jumanne eneo la al Bara , Bsida  na Maasaran Idlib na kusababisha maafa hayo.

Upinzani huo nchini Syria umelituhumu jeshi la Urusi kushambulia pia maeneo ambayo kulisainiwa makubaliano ya usitishwaji wa mapigano nchini Syria.

Mwanhabari wa shirika la habari la Uturuki Anadolu amesema kuwa wimbi la wahamiaji wanaoondoka katika eneo hilo baada ya mashambulizi imezidi kuongezeka .
 Habari Zinazohusiana