Zawadi ya fedha taslimu dola milioni 3 yawekwa kwa atakayemuua Rais Trump

Ahmed Hamza mbunge wa Kirman, eneo alikotokea jenerali Kasim Suleiman nchini Iran ametangaza bungeni watatoa dola milioni 3 kwa mtu atakayemuua Rais wa Marekani, Donald Trump

Zawadi ya fedha taslimu dola milioni 3 yawekwa kwa atakayemuua Rais Trump

Ahmed Hamza, mbunge wa Iran amesema watatoa zawadi ya dola milioni 3 kwa mtu atakayemuua Rais wa Marekani, Donald Trump.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran (ISNA), akiongea bungeni Hamza, mbunge wa Kehnuc mkoa wa Kirman, alisema kwa niaba ya watu wa Kirman ambako ndio eneo alikotokea jenerali wa Iran, Kasim Suleiman, aliyeuawa katika shambulizi lililopangwa na Marekani wameweka zawadi kwa kichwa cha Trump.

Hamza alisema,

"Kwa niaba ya watu wa Kirman tutatoa  zawadi ya fedha taslimu dola milioni 3 kwa mtu atakayemuua Trump”

 Habari Zinazohusiana