Kauli dhidi ya Ufaransa Ukanda wa Sahel zazidi kuongeza

Kauli dhidi ya Ufaransa Ukanda wa Sahel zazidi kuongeza

Kauli dhidi ya Ufaransa  Ukanda wa Sahel zazidi kuongeza

Kauli dhidi ya Ufaransa  Ukanda wa Sahel zazidi kuongeza
Eneo la Sahel Afrika Magharibi ni eneo ambalo limekumbwa na kusumbuliwa na vitendo vya kigaidi Barani Afrika katika miaka michache  iliopita.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa , idadi ya watu waliofariki katika mashambulizi ya kigaidi  nchini Niger, Burkina Faso na nchini Mali  imeongezeka tangu mwaka 2016 ambayo ilikuwa  770  na kufikia watu zaidi ya  4000 mwaka  2019 bila ya kuzungumzia wale ambao wamelazimika kuondoka katika makazi yao na kuwa wakimbizi.

Novemba mosi, askari 49 wa Mali waliuawa katika shambulizi la kigaidi lililolenga eneo la Indelimane. 
 

Shambulizi jingine liliendeshwa Disemba  17 Chinagoder ambapo ilitangazwa kuwa wanajeshi  80 waliuawa wa Niger.
Kutokana na mashambulizi hayo kutokea katika eneo moja imeonesha kwamba ni wazi kuwa kulikuwa na hitilafu na  myanya ambayo magaidi wanaweza kujipeneyeza na kuendesha mashambulizi na kufaanikiwa kusababisha hasara kubwa katika eneo hilo.
 

Kaskazini mwa Mali , eneo hilo  limeonekana kuwa kama  kitovu  cha ugaidi na maficho ambayo magaidi wanatumia kwa kuendesha shuhuli zao za kşgaidi.

Umoja wa Mataifa  umetuma kikosi chke cha kulinda amani ambacho  kina wanajeshi 10 000.

Ufaransa ambayo ina kamb yake nchini Niger, Mali na Chad  huwa jeshi lake hilo likiendesha mashambulizi na operesheni tofauti   dhidi ya makundi ya kigaidi tangu mwaka  2013.

Operesheni ya jeshi la Ufaransa iliopewa jina la Operesheni Serval  Kaskazini mwa Mali mwaka  2013 na baadae kuanzisha operesheni  nyingine ambayo ilipewa jina la Operesheni ya Barkhane, operesheni hiyo  ilianzishwa kwa ajili ya kukabilana na magaidi  Sahel mwaka  2014.
Chad mwaka 2014  na mataifa mengine katika ukanda kama Burkina Faso, Mali , Niger na Moritania zilikutana kuzungumziwa saula hilo  kwa pamoja ili kulinda usalama, muungano huo ulipewa jina la G5 Sahel .

Kwa pamoja katika muungano wa mataifa ya CEDEAO, Umoja wa Afrija  ulitakiwa kuingilia kati na kutafuta suluhisho na kuhakikisha amani katika ukanda mzima.  

Jambo hilo imekuwa wazi kuwa Ufaransa imekuwa ikionekana zaidi , jambo ambalo lilikuwa haliitajika katika Ukanda wakati watu wakihoji Umoja wa Afrika  wajibu wake ni nini? Ufaransa ni kama imechukuwa nafasi ya Umoja  huo.

Licha ya kuwa idadi kubwa ya  wanajeshi, tatizo la ugaidi nalo linazidi kuongezeka , kambi za jeshi la Ufaransa zimekuwa hazina maana yeyote na uwepo wake katika ukanda huo. Jambo hilo limepelekea kuliona jeshi la Ufaransa kama halina umuhimu wowote katika ukanda .

Ni wazi kuwa Ufaransa inatuhumiwa kuwa na ushirikiano na  viongozş ambao wanatuhumiwa kuwa madikteta na  vibaraka wa Ufaransa  kutokana na historia  ya ukoloni wa Ufaransa katika mataifa hayo Afrika Magharibi.

Uwepo wa Ufaransa na jeshi lake katika Ukanda huo umepelekea  kuibuka kwa hotuba na kauli dhidi ya ubepari wa Ufaransa kila kukicha katika mataifa ya Afrika Magharibi.


Tagi: Sahel , Ufaransa

Habari Zinazohusiana