Waziri mkuu wa Ethiopia amjibu Trump kuhusiana na tuzo ya Nobel

Kufuatia Rais Trump kuashiria kwamba yeye ndiye aliyestahiki kupewa tuzo ya Nobel, waziri mkuu wa Ethiopia atoa majibu

Waziri mkuu wa Ethiopia amjibu Trump kuhusiana na tuzo ya Nobel

Abiy Ahmed, waziri mkuu wa Ethiopia akiwa ziarani nchini Afrika kusini amejibu kuhusiana na madai ya RaisTrump wa Marekani kwamba yeye Rais Trump ndiye aliyestahiki kupata tuzo ya Nobel.

Abiy alisema kuwaambia wanahabari waliomuuliza juu ya suala hilo,

“Rais Trump alipaswa awalalamikie waandaaji wa tuzo za Nobel”. Aliongeza kwamba Rais wa Marekani hakupaswa kuelekeza malalamiko yake kwa Ethiopia bali alipaswa kuelekeza malalamiko hayo kwa kamati ya maandalizi ya tuzo hizo.

 " Sifahamu ni vigezo gani vinatumika kumchagua mtu wa kumpatia tuzo ya ".

Trump katika mkutano wa kampeni huko Ohio alisema ,

“ Nilifanya makubaliano Fulani, Nikaiokoa nchi moja. Lakini nasikia kwamba Kiongozi wan chi hiyo amepewa tuzo ya amani ya Nobel kwa kuiokoa nchi hiyo.”

Pamoja na kwamba Rais wa Marekani hakutaja jina la Ethiopia wala la Abiy waziwazi, lakini kauli zake hizo zilipingwa vikali nchini Ethiopia.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema Rais Trump alikuwa akizungumzia mgogoro baina ya Misri na Ethiopia uliotokana na mazungumzo juu ya Bwawa la umeme la Hedasi ambapo Marekani ilikuwa mpatanishi.

 Habari Zinazohusiana