Kwa mara ya kwanza Amir wa Qatar afanya ziara nchini Iran

Amir wa Qatar Shiekh Tamim bin Hamad al THani afanya ziara  yake ya kwanza nchini Iran

Kwa mara ya kwanza Amir wa Qatar afanya ziara nchini Iran


Amir wa Qatar Shiekh Tamim bin Hamad al THani afanya ziara  yake ya kwanza nchini Iran.

Amir wa Qatar kwa mara yake ya kwanza amefanya ziara rasmi nchini Iran Jumapili wakati ambapo ukanda upo katika hali ya hatari kufuatia mauaji ya jenerali wa jeshi la Iran nchini Irak, mauaji ambayo yaliendeshwa na jeshi la Marekani katika uwanja wa ndege wa mjini Baghdad na Iran kulipiza kisasi kwa  kushambulia kambi zake mbili.

Amir wa Qatar aliwasili mjini Tehran na kupokelewa na viongozi wa Iran.

Tamim amejielekeza nchini Iran akiwa na tume alioomgozana nayo katika ziara yake.
Ni mara ya kwanza amir wa Qatar kufanya ziara nchini Iran tangu kuingia madarakani mwaka  2013.

Taarifa zilizotolewa zi mefahamisha kwamba Al Thani amezungumza na rais wa Iran Hasani Rohani  na viongozi wengine wa ngazi za juu  nchini humo.

Ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili katika nyanja tofauti  umezungumziwa kuhakikisha utulivu.
 Habari Zinazohusiana