Iran yatangaza kujitoa katika mkataba wa nyuklia

Yabainisha haitatii kipengele hata kimoja katika mkataba wa nyuklia

Iran yatangaza kujitoa katika mkataba wa nyuklia

Iran imetangaza haitatii kipengele hata kitu kimoja katika mkataba wa nyuklia.

Taarifa ya maandishi iliyotolewa na serikali ya Iran inasema, Utawala wa Tehran kuanzia sasa hautatii kipengele hata kimoja kuhusiana na kurutubisha madini ya uranium, kuyahifadhi, kutafiti na kuendeleza.

Katika taarifa hiyo imeelezwa kuwa vinu vya nyuklia nchini Iran havitakuwa na idadi, itakuwa kadiri ya mahitaji ya nchi hiyo.

Taarifa hiyo ilisema kwamba Iran itaendelea kufanya kazi na taasisi ya kimataifa ya nishati ya nyuklia. Taarifa hiyo pia ilibainisha kwamba kama vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran vitaondolewa na maslahi yake yakizingatiwa Utawala wa Iran utakuwa tayari kurejea katika mkataba huo.


 


Tagi: nyuklia , mkataba , Iran

Habari Zinazohusiana