Wahamiaji haramu  782 wazuiliwa wakijaribu kuingia Ulaya

Wahamiaji haramu 782 wazuiliwa na kikosi cha kulinda mipaka cha Uturuki wakijaribu kuingia barani Ulaya

1325340
Wahamiaji haramu  782 wazuiliwa wakijaribu kuingia Ulaya

Wahamiaji haramu 782 wazuiliwa na kikosi cha kulinda mipaka cha Uturuki wakijaribu kuingia barani Ulaya
Wahamiaji haramu takriban 782 waripotiwa kuzuiliwa na kikosi cha kulinda mipka cha  Uturuki waliokuwa wakitaka kuvuka mpaka kinyume na sheria na kuingia barani Ulaya.
Wahamiaji waliokamatwa ni raia kutoka nchini Moroko, Sudani, Afghanistani, Bangladesh, Pakistani, Syria, Iraq na Algeria.
Wahamiaji hao wamekatwa  mkoani Edirne, mkoa ambao unapatikana  Kaskazini-Magharibi mwa  Uturuki  mpakani mwa Uturuki, Ugiriki na Bulgaria.
Msako mkali umeendeshwa katika vitongoji tofauti baada ya kukamatwa wahamiaji hao  katika  eneo la Ipsala na Meriç.
Wahamiaji waliokamatwa ni raia kutoka nchini Moroko, Sudani, Afghanistani, Bangladesh, Pakistani, Syria, Iraq na Algeria.
Baada ya kukamatwa kwa wahamiaji hao , kituo cha kusajili wahamiaji  kimewapokea kwa ajili ya usajili wa kisheria.
 Habari Zinazohusiana