Rais Erdoğan akerwa na wanaouhusisha Uislamu na Ugaidi

Rais Recep Tayyip Erdoğan, amesema, walaaniwe wale wote wanaouhusianisha uislamu na ugaidi

Rais Erdoğan akerwa na wanaouhusisha Uislamu na Ugaidi
erdogan.jpg
erdogan.jpg

Rais Recep Tayyip Erdoğan, amesema walaaniwe wale wote wanaouhusianisha Uislamu na ugaidi.

Erdoğan, ambaye yupo jijini London katika mkutano wa viongozi wa mataifa ya NATO alikutana na raia wa Uturuki na jumuiya ya waislamu.

Katika mkutano huo Erdoğan alisema,

“Kutokea hapa kupitia ninyi natuma salamu zangu kwa wadhulumiwa  ambao mioyo yao ipo na sisi ndugu zetu wa Asia, Afrika, Turkistan, Kashmir, Myanmar, Yemen, Libya, Syria. Mapenzi yangu makubwa kwa ndugu zangu wa Palestina ambao wanatetea kibla yetu ya kwanza kwa gharama ya damu zao”.

Erdogan aliendelea kwa kusema,"Leo hii ukilinganisha na miaka 17 iliyopita Uturuki ipo imara zaidi. Leo hii Uturuki inayochezewa kirahisi rahisi haipo, Ipo Uturuki iliyothabiti inayopanga na kuvuruga mipango katika kanda. Leo haipo Uturuki inayofungua mikono kwa bilioni kadhaa za dola. Hivi sasa ukilinganisha na pato la nchi yake, Uturuki ndio taifa linaoongoza kwa kutoa misaada. Leo hii ukilinganisha na mwaka 200 uchumi umekuwa mara 3.5. Wastani wa kipato kwa kichwa umeongezeka kutokan dola elfu 3 na 500 mpaka kufikia dola elfu 9 na 700. Leo hii Uturuki inavunja rekodi kila mwaka katika mauzo ya nje. Leo hii ipo Uturuki ambayo ina miundombinu ya kisasa kabisa, Ina mmoja miongoni mwa viwanja vya ndege vikubwa vitatu duniani. Ipo Uturuki ambayo imekamilisha miundombinu inayounganisha Ulaya na Asia.Leo hii ipo Uturuki ambayo inatetea haki zake kutokea Ege, Karadeniz na mashariki mwa Mediterenan, Uturuki ambayo inalinda maslahi yake na yenye nguvu za kijeshi”.

İslam ni neno la kiarabu linalomaanisha  ''amani'' limezaliwa kutokana na neno "silm"  akikumbushia Rais Recep Tayyip Erdoğan, aliendelea kwa kusema,

"Uislamu ni dini ya amani, Dini yetu ambayo ni dini ya amani hamuwezi kuihusianisha na ugaidi wala hamuwezi kuiweka sifa ya uislamu katika ugaidi. Kwa wale wote wanaotumia maneno haya waniwie radhi, na mimi pia naomba walaaniwe. Watu hao wanatakiwa waulizwe haya. Aliyeuwa waislamu 51 wakiwa katika ibada mnamo mwezi Machi nchini New Zealand ni nani ? Mkristo. Je sisi tumesema hata mara moja kama Ukristo ni ugaidi? Tumetumia maneno ya namna hiyo hata mara moja ?, Hatujatumia. Na hatujatumia kwa vile dini yetu ya Uislamu hairuhusu jambo hilo. Cha kwanza tuzungumze ni jinsi gani tunaweza kuleta amani miongoni mwa dii zetu. Kwa bahati mbaya katika dunia ya sasa kuna baadhi ya viongozi waliokosa heshima kutoka katika mataifa yanayoheshimika wamekuwa wakitamka kwamba uislamu ni ugaidi. Suala hili haliwezekani. Hatuwezi kukubaliana na hili. Tumeshawaambia mara nyingi  tunaendelea kuwaambia msitumie matamshi hayo katika mazungumzo baina yetu, mnatuumiza "

 Habari Zinazohusiana