Putin aikosoa Marekani

Rais Putin ameikosoa Marekani kutokana na mpango wake wa kwenda kufanya oparesheni ya kijeshi katika anga la mbali

Putin aikosoa Marekani

Rais wa Urusi, Vladmir Putin, amezungumzia kuhusu mpango wa Marekani kuunda kikosi cha jeshi kwa ajili ya oparesheni katika anga za mbali,

“Uratibu wa siasa za kijeshi za Marekani , mpango wa kufanya oparesheni za kijeshi katika anga la mbali vinaonekana kama mchezo wa kuigiza” alisema Putin.

Putin alizungumzia mpango huo wa Marekani wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa jeshi la majini la Urusi uliofanyika mjini Sochi.

Mataifa makubwa yamebuni mifumo ya kijeshi ya kisasa kwa ajili ya oparesheni za kijeshi angani na wameiboresha mifumo hiyo. Marekani imepanga kufanya oparesheni za kijeshi katika anga la mbali.

Putina alisema, “ Uratibuwa siasa za kijeshi za Marekani na mpango wake wa kufanya oparesheni za kijeshi katika anga la mbali vinaonekana kama vile maigizo”
 

Putin alisisitiza kwamba Urusi inapinga suala la kufanya oparesheni za kijeshi na kuweka  silaha katika anga za mbali, vilevile ipo kinyume na uendelezwaji wa mifumo ya kielektroniki ya kijeshi.

 Habari Zinazohusiana