Watu 79 wamekamatwa katika maandamano nchini Iran

Idara ya upelelezi nchini Iran imetangaza kuwakamata watu 79 wakihusishwa na maandamano nchini humo

Watu 79 wamekamatwa katika maandamano nchini Iran


Idara ya upelelezi nchini Iran imetangaza kuwakamata watu 79 wakihusishwa na maandamano nchini humo.

Watu 79 wameripotiwa kukamatwa katika maandamano nchini Iran, maandamano ambayo yalizuka ikifahamishwa kuwa waandamanaji wanapinga kupandishwa kwa bei za mafuta.

Mamlaka ya Huzistan nchini Iran imefahamisha Jumatatu kuwa watu 79 ndio waliokamatwa  kufuatia maandamano.

Taarifa ilitolewa na vyombo vya habari nchini Iran imesema kuwa  watu waliokamatwa wanatuhumiwa kuharşbu mali ya umma na mali za watu binafsi katika maandamano.

Msako ulioendeshwa, maafisa wa usalama wamesema kuwa  silaha zimekamatwa .
Maandamano hayo kulingana na wadadisi wa masuala ya kisiasa yamesababishwa na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.

Maandamano hayo ya kupinga kupanda kwa bei za mafuta yalianza Oktoba 15 nchini Iran.

Shirika la Amnesty International limefahamisha kwa upande wake kuwa watu 161  wameuawa katika maandamano.Habari Zinazohusiana