Mzee huyu wa Japan atakuacha mdomo wazi

Apiga simu kituo cha huduma kwa wateja mara elfu 24, polisi wamtia nguvuni

Mzee huyu wa Japan atakuacha mdomo wazi

Mwanaume alipiga simu mara elfu 24 katika kituo cha huduma kwa wateja cha shirika la simu, KDDI, nchini Japan ametiwa nguvuni.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka Japan, Polisi mjini Tokyo wamemkamata Akitoshi Okamoto mwenye umri wa miaka 71 kwa tuhuma za kuvuruga kazi katika kituo cha huduma kwa wateja cha shirika la simu la KDDI. Mzee huyo inasemakana alipiga simu mara elfu 24 kutokana na mkataba aliosaini kuvunjwa na hivyo alikuwa anataka aombwe radhi.

Akitoshi alikuwa akiwatukana wafanyakazi wa kituo hicho cha huduma kwa wateja mara wakipokea simu na mara nyingine simu ilipopokelewa tu alikata.

 


Tagi: Japan , KDDI

Habari Zinazohusiana