Erdoğan : "TANAP ni mradi unaoashiria mtazamo wa amani wa Uturuki "

Mradi wa bomba la kusafirisha gesi TANAP ni ishara tosha kuwa Uturuki ina mtazamo wa amani ya kudumu

Erdoğan : "TANAP ni mradi unaoashiria mtazamo wa amani wa Uturuki "

 

Mradi wa bomba la kusafirisha gesi TANAP ni ishara tosha kuwa Uturuki ina mtazamo wa amani ya kudumu.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa mradi wa bomba la kusafirissha gesi wa TANAP ni ishara tosha kuwa Uturuki ina mtazamo na malengo ya amani ya kudumu katika ukanda.

Rais Erdoğan ameshiki katika hafla ya ufunguzi wa mradi huo wa TANAP katika kituo cha TANAP MS4 ilioandaliwa Ipsala mkoani Edirne.

Katika hafla hiyo, rais Erdoğan amezungumza akisema kuwa tukio hilo ni tukio la kihistoria ambalo pia Uturuki imewajibika kwa kiasi kikubwa.

Rais Erdoğan ameendelea akisema kuwa mradi huo ni ishara ya malengo ya amani ambayo Uturuki imejitolea katika ukanda.

TANAP ni mradi ambao una umuhimu mkubwa katika ukanda kutoka nchini Azerbaijani katika eneo la kilomita 3500 kuelekea barani Ulaya.

Juhudi kubwa za Uturuki zilioneka tangu kuanza kwa mradi huo Juni mwaka 2012 na sasa ni wazi kuwa mradi huo unaendelea kama ulivyokuwa umepangwa kuendeshwa.

Rais Erdoğan amegusia pia kuhusu hali ya mvutano uliopo katika Bahari ya Mediterania Mashariki kwa kusema kuwa Uturuki itaendelea kutetea haki za waturuki ya Jamhuri ya Kupro Kaskazini na kamwe haitofumbia macho pindi haki zao zitakuwa hatarini.

Rais Erdoğan amekemea baadhi ya viongozi ambao wanachochea kuchomwa utambi badali ya kutafakari namna ya kuchangia rasilimali zinazopatikana katika bahari hiyo.

Ni jambo la kushangaza kuona kukitumiwa lugha za vitisho wakati suluhisho lipo wazi na ni jambo linalowezekana.Habari Zinazohusiana