Je suala ni mtazamo wa ki Ottomani ?

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL  mkuu wa kitivo cha siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anafafanua kuhusiana na mitazamo iliopo juu ya dola la Ottomani

1267081
Je suala ni mtazamo wa ki Ottomani ?

Kuna baadhi ya mada ambazo haitoshi tu kuwa sahihi bali yapasa kupatia ufumbuzi changamoto. Moja ya mada hizo ni urithi ulioachwa na serikali ya dola la Ottomani. Mara zote suala la dola la Ottomani litazamwe vipi limekuwa suala la mjadala. Mara ya mwisho Rais wa Lebanon, Michel Aoun, katika kuadhimisha miaka 100 ya kuanzishwa kwa taifa hilo alisema kwamba kwa msaada wa Wafaransa walipata uhuru wao huku akilituhumu dola la Ottomani kwa kufanya ugaidi katika taifa hilo.

Tuhuma hizohizo pia utazikuta katika vitabu vya kiada na ziada vya magharibi na baadhi ya mataifa ya kiarabu.

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL  mkuu wa kitivo cha siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anafafanua kuhusiana na mada hii...

Kwa utawala ambao umedumu kwa miaka 600 ukiongoza serikali, bila shaka unaweza kuwepo ukosoaji wa kila aina katika kila nyanja.

Lakini shutuma za uvamizi na ukandamizaji  dhidi ya utambulisho na tamaduni mbalimbali ambazo zinaweza kuelekezwa kwa mataifa ya kibeberu, itakuwa ni fitina za waziwazi kuzielekeza shutuma hizo kwa dola la Ottomani.

Uturuki kwa namna fulani kwa kushindwa kufanana na dola la Ottomani inakosolewa kwa kushindwa kwa sera za kujinasibisha na dola hilo.

Ingekuwa dola la Ottomani lilitumia sera za kiuvamizi na kiukandamizaji basi maeneo mengi yaliyotawaliwa na dola hilo hivi sasa zingekuwepo athari yaani katika maeneo hayo kungekuwepo na uuturuki na uislamu zaidi.

Zana hii ni ya msingi kwani maeneo ambayo yalitawaliwa na waingereza na wafaransa yanaonekana ni kwa jinsi gani hii leo yanafanana na mataifa hayo.

Tukumbushie tu kwamba moja ya tofauti kubwa katika mtindo wa utawala baina ya dola la Ottomani na mataifa ya kibeberu ni kutotumia siasa za uvamizi na ukandamizaji.

Amani ya ki ottomani “Pax Ottomana”

Maeneo mengi ya kijiografia ambayo yalikuwa chini ya utawala wa dola la Ottomani kwa karne nyingi hivi sasa ni bahari za damu.

Balkani, mashariki ya kati na Afrika kwa karne nyingi yalikuwa katika amani yakitawaliwa kwa kuheshimu dini, tamaduni na mila mbalimbali kitu ambacho hivi sasa kimeshindikana.

Hali hio ni mfano halisi kwamba katika kipindi cha utawala wa dola la Ottomani, tofauti zote za dini, makabila, lugha ziliruhusiwa ziendelee kuwapo. Katika rejea, uvumilivu huo wa dola la Ottomani unafahamika kama Pax Ottomana ( Amani ya ki Ottomani).

Thamani ya uwepo wa tofauti uliovumiliwa na kuachwa udumu katika maeneo husika yaliyotawaliwa na dola la Ottomani ni bora zaidi ukilinganisha na uvamizi uliofanywa na Marekani baada ya kuanzishwa, katika maeneo mbalimbali iliyotawala ilifuta dini, na makabila ya maeneo hayo; Pamoja na Uingereza kutawala bara hindi kwa miaka 150 pekee utaona kwamba mataifa yote yaliyoanzishwa katika eneo la utawala la bara hindi  lugha rasmi ni kiingereza.

Ingekuwa dhana ya kwamba dola la Ottomani lilitawala kwa mabavu na ukandamizaji kama vile mataifa mengine ya kibeberu basi jina la Rais wa Lebanon lisingekuwa “Michel Aoun”  na ingekuwa ngumu kuwepo kwa ukristo eneo hilo.

Mwandishi  Amin Maalouf katika moja ya kazi yake muhimu anatoa maelezo kwa walebanon kama yeye na ambao ni wakristo kuhusiana na ukosoaji wao juu ya sera za dola la Ottomani, maneno yake  ni kama vile yanamjibu  Rais wa nchi yake: “ Hakuna dini inayokataza uvumilivu. Lakini kama ukilinganidha hizi dini mbili pinzani, basi Uislamu hauwezi kuonekana mbaya kwa vyovyote vile. Ingekuwa mababu zangu katika nchi ambazo zimevamiwa na majeshi ya kiislamu wangelazimishwa kubadili dini zao kutoka ukristo kuwa waislamu wasingeweza kutetea dini zao kwa karne 14, sizani kama wangeweza kuendelea kuishi katika vijiji na miji yao. Ni kipi kiliwakuta waislamu wa Uhispania? Au nini kiliwakuta waislamu wa Sicily ?, walitokomezwa, waliuawa hadi mtu wa mwisho, walilazimishwa kuyahama maeneo  yao au wabadili dini zao kuwa wakristo.

Naye profesa wa historia wa kiyahudi Yuval Noah Harari, katika moja ya makala zake maarufu alizoandika katika gazeti la Hürriyet hivi karibuni alielezea Pax Ottomana na kuonyesha uvumilivu wa dola la Ottomani kwa maneno yafuatayo:

“Katika zama za kati hakukuwa na uvumilivu barani Ulaya... mwaka 1600 Paris kila mtu alikuwa mkatoliki. Akiingia katika mji wa waprotestant aliuawa. London kila mtu alikuwa mprotestant. Akiingia katika mji wa wakatoliki aliuawa. Miaka hiyo wayahudi walikuwa wakifukuzwa barani Ulaya... Hakuna aliyetaka kumuona muislamu... Lakini katika kipindi hicho hicho Istanbul madhehebu mbalimbali, waislamu, wakatoliki, waarmenia, waortodox, warumi, wabulgaria n.k walikuwa wakiishi pamoja bega kwa bega raha mustarehe.”

 

Kutumika kwa Historia au kuendelea kuligawa eneo la kihistoria la dola la Ottomani...Shutuma dhidi ya dola la Ottomani, ziwe kama tulizozitaja hapo juu au nyingine zinaweza kutolewa majibu mengi. Lakini suala sio kutolea tu majibu shutuma hizo. Suala hapa ni mikakati ya kibeberu “ Gawanya, bagua, tawala”.Sifa kuu ya Uislamu ambao ulizuia kwa miaka mingi ubaguzi na hivyo kudumisha amani ,suala la kama hivi sasa sifa hiyo inaweza kutumika tena inaweza kukubaliwa au isikubaliwe. 

Bado inahitajika  nchi zilizopo katika jiografia ya Ottomani (Balkan, Mashariki ya kati, Afrika) ziendelea kugawanyika. Kwa kutumia tofauti ndogo ndogo za kikabila, kidini, kiutamaduni na utambulisho mwingine mpya ulioibuka kitaifa wanaendelea kuligawanya zaidi eneo hili la kijiografia.

Na hio ndio sababu kuu ya kuendelezwa migogoro na oparesheni za kuchora mipaka mipya. Katika muktadha huo nyenzo za kihistoria za kibeberu zinahitajika kutumika. Katika hilo historia tuwaachie wanahistoria.

Hakuna anayepinga kutumia historia, katika hilo beberu ambaye hutumia chochote kile mradi tu atimize malengo yake, tutakubali vipi kwamba beberu huyo ataacha kuitumia historia kwa maslahi yake?.

Katika hali hiyo nini kifanyike?

Ni kwa ajili hiyo tathmini siyo kutathmini kama urithi kutoka katika dola la Ottomani umepitwa na wakati au ni sehemu ya historia.

Inabidi kufunza msimamo utaohusu leo na kesho.Hatuwezi kusema kwamba wanataaluma wa ki Ottomani na wale wa Jamuhuri kuhusiana na mada hii wametoa mtihani mzuri kwa wanasiasa, hii inatokana na wengi  wanasiasa hawa kuathiriwa na virusi vya umagharibi.

Wanataaluma na wanasiasa ambao kutokana na umagharibi wametenganishwa na tamaduni na maadili ya jamii zao wamefanywa kuwa mawakala wa fikra za kimagharibi za kuendelea kuligawa eneo hili.

Leo hii mtazamo wa wanataaluma na wanasiasa, waliopitia katika chujio la mataifa mengine la kumagharibisha, kuhusiana na dola la Ottomani na jamii zao hauna tofauti na hali hio.

Kiuhalisia hali ya sasa ya Balkan, Mashariki ya kati na Afrika haina tofauti na ile ya zamani. Nchi hizi kila uchwao zimekuwa zikikumbwa na hatari ya kugawanya zaidi. Wanasiasa na wanataaluma ambao wameoshwa akili zao, ambao wametanganishwa na tamaduni, mila, desturi na maadili yao hawawezi kuziongoza jamii zao katika eneo jingine isipokuwa kuzigawa zaidi.

Ni kwa ajili hiyo kwa kufahamu vizuri malengo ya mabeberu tunapaswa kuingalia historia  ya kale na ya sasa katika hali ambayo italeta amani zaidi katika jamii na eneo.  

Wanataaluma, wasomi, waalimu, watu wa busara, wanasiasa na watu wote wenye akili timamu kutoka maeneo yote wanapaswa  kuwa na msimamo na mtazamo wa pamoja na kupinga kwa nguvu zote utumikaji wa historia kama nyenzo kwa mazumuni ya kugawanya zaidi.  

Wasiangalie tu kwa kutumia dirisha waliloonyeshwa bali watazame madhumuni hasa ya kisiasa. Wanapaswa zaidi kutafuta milango ya fikra za ndani zinazotokana na historia, tamaduni na mila zetu wenyewe zenye lengo la kuweka pamoja kuliko kutegemea fikra kutoka nje zenye lengo la kugawanya zaidi.

Vinginevyo watu na mataifa ya eneo  kwa kuendelea kugawanywa, yatashushana yenyewe kwa yenyewe, yatakosa nguvu na kushindwa kujitawala, kitu ambacho kitapelekea kuendelea kuwa wanasesere wa mabeberu.  

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL  mkuu wa kitivo cha siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt

 Habari Zinazohusiana