Je unapochukua teknoloji unachukua pia na utamaduni ?

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha siasa  chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anafafanua kuhusiana na mada hii ya uhusiano baina ya teknolojia, mila, desturi na utamaduni

1263040
Je unapochukua teknoloji unachukua pia na utamaduni ?

Nchini Uturuki na katika dunia ya waislamu kwa miaka 200 kumekuwa na mjadala juu ya fasili za maneno mila, tamaduni na teknolojia. Katika siku za hivi karibuni inaonekana mjadala juu ya teknolojia umepamba moto.Teknolojia ni zaidi ya mbinu mpya na ufundi hujumuisha pia utamaduni na mambo mengine mengi yasiyo takikana yanayokwenda sanjari na teknolojia. Ni kwa minajili hiyo hata kama ukijitenga kutokana na teknolojia, mtazamo bado utaendelea.

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha siasa  chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anafafanua kuhusiana na mada hii...

Ni nini cha kuchukua kutoka Magharibi ?

Awali ya yote tuweke wazi kwamba mjadala sio tu juu ya teknolojia mpya. Nini tuchukue au tusichukue kutoka magharibi pia ni sehemu ya mjadala.Katika miaka ya mwisho ya dola la Ottomani mada hii imejadiliwa kwa kina na waandishi tofauti mfano maendeleo ya vitu- maendeleo ya maadili (Said Halim Paşa), ustaarabu-utamaduni (Ziya Gökalp), utamaduni wa kihalisia na kinadharia(Celal Nuri) n.k.

Tunaweza kusema shairi la Akif liliandikwa katika muktadha wa mjadala huo.

“Umepata elimu umepata sanaa ya mavazi

Umetoa muda na kasi yako ya mwisho

Kwa sababu  kuishi kunategemea mambo hayo

Kwa sababu sanaa haina utaifa”

Kipindi cha uhuru fikra za baadhi ya waturuki na baadhi ya waislamu ilikuwa ni kwamba elimu ya magharibi ichukuliwe ila desturi, mila na tabia zao waachiwe wenyewe.

Kuhusiana na maada hii mnaweza kurejea makala yangu “ Msimamo gani  dhidi ya magharibi ni muafaka”.

Baadae Akif na wenzie walikosoa kutojifunza vizuri na vya kutosha kutoka magharibi. Mimi ni mmoja wanaofikiri kwamba Akif hakutendewa haki kwa kuwa  sidhani kwamba ukosoaji wa Akif juu ya masuala yafutayo haukuonekana.

Uhusiano baina ya teknolojia na Utamaduni

Bila shaka teknolojia inaakisi kilichozaliwa na utamaduni wa kiujumla wa jamii. Je inawezekana kufikiri kwamba utamaduni ulio ndani ya teknolojia ya kumuumba mwanadamu upya kupitia akili bandia unajitegemea ? sizungumzii utamaduni wa magharibi. Hivi sasa hata mataifa kama China yaliyo mbali na jamii za magharibi kunatengenezwa aina hiyo ya teknolojia.

Mabomu ya nyuklia ambayo zaidi ya kuangamiza jeshi la adui huangamiza makumi kwa maelfu ya raia wa eneo yaliyolipuliwa, huangamiza pia mimea na viumbe hai vingine na kufanya ardhi za maeneo husika kutomea chochote, Je inawezekana vipi kutenganisha akili za waliotengeneza teknolojia hio na teknolojia yenyewe?.Mtazamo tofauti na fikra hizo unaonekana kwa Kanuni Sultan Süleyman, inawezekana kutolewa mifano tofauti ya uhusiano baina ya teknolojia na utamaduni. Kanuni alikuwa akichukizwa nna kitendo cha siafu kukausha miti katika bustani ya kasri lake. Lakini kwa kujua kuwa siafu hao pia ni viumbe hai, kuhusiana na hilo ikabadi amuulize mtukufu Şeyhülislam Ebussuud kwa njia ya shairi:

“Miti ya matunda yakaushwa na siafu

Je kuna madhara kuwakausha siafu”

Mtukufu Ebussuud  naye kwa njia ya shari akatoa jawabu ambalo linatoa mtazamo wa wazi wazi juu ya uhusiano tofauti wa teknolojia na utamaduni:

 “Itakapofika kesho katika kisimamo cha haki

Atadai siafu kutoka kwa Suleiman yake haki”

Mitazamo yote miwili ya teknolojia inayozalishwa na  teknojia hii iliyozalishwa inapoupeleka ubinadamu, bila shaka itakuwa tofauti. Ughaibu unaokuja kutokana na teknolojia nalo ni suala ambalo linapaswa kutizamwa.

Teknolojia ipi ?  

Pamoja na kwamba ni ukweli usiopingika kwamba teknolojia ina uhusiano na utamadani, tamaduni mbalimbali zinakubaliana na fikra kwamba mazao ya teknolojia ni hasi na yenye madhara kwa namna fulani. Kila tamaduni imekuwa ikizalisha teknolojia itakayoiwezesha kukidhi mahitaji yake.Mjadala unaweza kuwa mahitaji ni nini au ni yapi.  Lakini haiwezi kusemwa kwamba  mahitaji ya binadamu hayawezi kutoshelezwa kwa muingiliano wa tamaduni tofauti. Ni kwa ajili hiyo leo hii watu kutoka katika tamaduni tofauti wamekuwa wakitumia teknolojia zinazofanana.

Ni kwa ajili hiyo hatuwezi kutazama teknolojia zinazozalishwa katika tamaduni tofauti katika mtazamo wa kiujumla na wa kubagua.

“Tafuteni elimu hata ikiwa ni Uchina”. “Hekima ni mali ya muumini iliyopotea”. “Andaeni silaha madhubuti dhidi ya maadui zenu”, “ Muislamu mwenye nguvu ni bora zaidi kuliko muislamu dhaifu”. Hadithi hizo za mtume zinatuusia kuwa makini na waangalifu juu ya suala la teknolojia.Zinatutaka tuwe hai katika kutafuta teknolojia. Andaeni silaha madhubuti dhidi ya maadui zenu, isituingize  katika kuangamiza nchi nyingine kwa mabomu ya nyuklia kwa kuwa sisi ni waislamu. Vivyo hivyo pia kwa wale wanaofikiri tunaweza kuchukua teknoloji hii wasitoe kipaumbele kwa suala hilo.

Inapendekezwa nini ?

Wanaoitazama teknolojia kwa mtazamo hasi tofauti na makundi mengine hawatoi mapendekezo mbadala ya kihalisia. Kwa ujumla wanakubalina na dhana kwamba teknolojia ya magharibi ni muendelezo wa fikra, imani na falsafa za magharibi. Ukosoaji wa watu hao bila shaka unaamsha aina fulani ya kuwa waangalifu. Lakini muenendo ambao uko finyu sana kinyume na falsafa ya “ Tafuteni elimu hata kama ni Uchina” .Watetezi wa fikra hiyo ya kiujumla au yenye makatazo huweza kutumia siasa kali sana katika utetezi wao. Kuikataa kiujumla teknoloji iliyotengenezwa au ambayo haijatengenezwa kunaweza kutengeneza jamii ambayo imejifungia na yenye siasa kali. Upande mwingine unaruhusu matumizi ya kimsingi ya teknolojia au kutengeneza teknolojia ambazo ni muhimu katika kuwezesha na kurahisisha maisha ya kila siku ya muislamu. Bila shaka mapendekezo hayo ni ya thamani. Katika jamii ambayo inataka kutumia kila kitu kwa fujo , pendekezo la kubana matumizi na kutumia kila kitu kwa kiasi inakuwa ni pigo. Bila shaka waislamu wanapaswa kufanya juhudi katika kuzalisha teknolojia zitakazowawezesha wao na waislamu wengine kuishi salama. Mapendekezo ya namna hio yana maana kubwa. Lakini juhudi zozote za kujifungia na kujiweka mbali na ulimwengu zinaweza kupelekea matumizi ya njia za kigaidi, mifano inaonekana katika mataifa mengi ya kiislamu.

Dunia ya kiislamu sio yenye kutumia sana teknolojia kwa wakati tuliopo. Na wala haijajaribu kutumia teknolojia kwa uchache zaidi. Katika sheria ya mwaka 1838 kuhusiana na makubaliano ya kibiashara ya bandari ya Balta, kuliwekwa vikwazo vikali  na marufuku katika kuingiza nchini mali kutoka mataifa ya kigeni. Mgomo  baridi wa Gandi huko India, kukataliwa teknoji ya amish huko Marekani ni mambo ambayo yanafahamika. Katika hatua tuliyofikia ikiwa tunazungumzia juu ya ubeberu wa kimagharibi na uibukaji wa nguvu mpya, ni wazi kwamba pendekezo la kujitenga na maendeleo ya kidunia halitatoa njia mbadala. Njia hizo zinaweza kudhoofisha mfumo wa uzalishaji wa kibepari. Lakini ubepari hauwezi kuondoa ubabe uliopo hivi sasa magharibi ambao kesho unaweza kubadilika.

Kupinga uwoga dhidi ya teknolojia

Kama mashaka dhidi ya teknolojia yanatokana na mipaka tuliyozungumzia hapo juu yanaweza kueleweka, kinyume na hapo kupinga teknolojia itakuwa ni kujifungia, kujirudisha nyuma na kukaribisha kupoteza uhuru.Uoga dhidi ya teknolojia au upingwaji wake ni mwenendo wa kujisalimisha uliojengwa katika misingi ya kwamba hakuna teknoloji ya manufaa kwa binadamu inayoweza kutengenezwa.

Kama hitimisho madhara yanayotokana na teknolojia, ukosoaji kwamba teknolojia zitaangamiza kizazi cha mwanadamu, ni masuala ambayo yanazikumba jamii zote. Cha msingi ni kuwa na tabia ya kuziangalia kwa makini hizi teknolojia. Inawezekana ikaonekana ni jambo la busara kuzipinga kiujumla moja kwa moja teknolojia bila kubagua. Lakini kupinga kinachowezekana na kuonyesha mfano wa kinadharia kama suluhisho huweza huondoa suluhisho linalowezekana, na mtazamo huo unaweza kutumika kukumbatia na kueneza zaidi kile kinachopingwa.

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha siasa  chuo kikuu cha Ankara Yıldırım BeyazıtHabari Zinazohusiana