Facebook kuja na pesa mpya ya kidigitali

Mtandao wa kijamii wa Facebook umetangaza kuanzia mwaka 2020 itaingiza sokoni pesa ya mpya ya kidigitali ijulikanayo kama "Libra"

1222274
Facebook kuja na pesa mpya ya kidigitali

Mtandao wa kijamii wa Facebook umetangaza kuingiza sokoni pesa mpya ya kidigitali sokoni.

Tangazo hilo kutoka Facebook linasema pesa hiyo mpya ya kidigitali itayoingizwa sokoni mwaka 2020 itaitwa “Libra”.Pesa hio pia itakubalika katika mifumo ya malipo kama vile Visa na Mastercard.

Taarifa hiyo inasema baada ya kuingizwa sokoni pesa hiyo ya kidigitali itaanzishwa pia pochi ya kidigitali ya kuhifazia pesa hio iitwayo “Calibra”. Taarifa hiyo inasema huduma hiyo kwa watumiaji itawezesha kuokoa pesa pia matumizi na kutumiana pesa miongoni mwao.

Katika taarifa hiyo ya Facebook imekumbushia kwamba pesa hiyo ya kidigitali na pochi ya kidigitali vitaweza kutumiwa katika na mtu yeyote ambaye kwenye simu yake ana program tumizi za  Facebook Messenger, WhatsApp au “Calibra”.Habari Zinazohusiana