Ufaransa yaipendekezea Uturuki kununua mfumo wa kupambana na makombora Samp-T

Waziri wa ulinzi wa Uturuki afahamisha kwamba Ufaransa yaipendekezea Uturuki kununua mfumo wa Samp-T

Ufaransa yaipendekezea Uturuki kununua mfumo wa kupambana na makombora Samp-T

Waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar asema kwamba Ufaransa  imelipendekezea jeshi la Uturuki kununua mfumo wa kukabilaina na makombora wa Samp-T na kuufanyia uchunguzi Kahramanmaraş katika kambi ya Incirlik inayopatikana mkoani Adana.

Akar amewaambia waandishi wa habari kuwa Ufaransa imependekezea Uturuki kununua mfumo huo ambao ni wa masafa ya mastani katika kukabiliana na makombora wa Samp-T.

Waziri  wa ulinzi wa Uturuki amesema kuwa pendekezo hilo  litafanyiwa kazi.

Katika taarifa hiyo, Hulusi Akar amefahamisha kwamba tayari  jeshi la Uturuki  limekwishateua wanajeshi  ambao wamekwishachaguliwa kujielekeza nchini Urusi  kupatiwa mafunzo kuhusu mfumo wa kujihami na makombora wa S-400.Habari Zinazohusiana