Wapalestina waendelea kukamatwa na askari wa Israel

Askari wa Israeli wamekamata Wapalestina 10 katika eneo la West Bank.

Wapalestina waendelea kukamatwa na askari wa Israel

Askari wa Israeli wamekamata Wapalestina 10 katika eneo la West Bank.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na jeshi la Israeli, Wapalestina 10 wametiwa kizuizini kwa madai ya "kushiriki katika vitendo vya kigaidi" katika mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya Magharibi mwa eneo hilo la Ukingo wa Magharibi.

Majeshi ya Israeli, ambayo mara kwa mara yamekuwa yakivamia nyumba za Wapalestina katika eneo la West Bank na Mashariki mwa Yerusalemu na kuwafunga kwa madai mbalimbali.

Baadhi ya Wapalestina, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, wamekuwa katika magereza hayo kwa muda .

Kulingana na vyanzo rasmi vya habari  nchini  Palestina, kuna Wapalestina 5,500 katika magereza ya Israeli, 230 kati yao wakiwa ni watoto.
 Habari Zinazohusiana