Trump ainyooshea kidole cha lawama Mexico kuhusu wahamiaji

Rais wa Marekani Donald Trump aitupia lawama Mexico kufumbia macho suala zima la wahamiaji

Trump ainyooshea  kidole cha lawama Mexico  kuhusu wahamiaji

Donald Trump, rais wa Marekani ameitupia lawama Mexico kuhusu wahamiaji akisema kwamba Mexico  haikuwajibika ipasavyo dhidi ya wahamiaji.

Trump kufuata suala la wahamiaji amesema kuwa Mexico ilifanya kosa na itarajie jibu linalostahili  kutoka kwake.

Trump ameituhumu moja kwa moja Mexico kufumbia macho  suala la wahamiaji haramu kutoka Amerika Kusini kupitia Mexico na kuingia kinyume cha sheria katika ardhi ya Marekani.

Kwa mujibu wa Trump, Mexico haikuwajibika ipasavyo kulinda mipaka yake na kuwazuia wahamiaji.

Kulingana na mashirika ya kutetea haki za binadamu, raia kutoka katika mataifa tofauti Amerika Kusini kama Guatemala, Honduras na El Salvador walijaribu kuvuka mpaka kati ya Mexico na Marekani baada ya kuingia nchini Mexico kinyume cha sheria wakikimbia  hali ngumu ya maisha katika mataifa yao.

Rais Trump katika sera zake za kukabiliana na wahamiaji haramu na biashara haramu ya madawa ya kulevya, ameendelea kuunga mkono  juhudi zake za kutaka ujengwe  ukuta kwa ajli ya kuwazuia wahamiaji haramu na walanguzi wa madawa ya kulenva kuingia nchini Marekani.Habari Zinazohusiana