Mvutano baina ya Marekani na Iran

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt

Mvutano baina ya Marekani na Iran

              İbni Haldun, mwana falsafa mkubwa wa kiislamu alifananisha mataifa na watu, kama ilivyo kwa watu mataifa nayo huzaliwa, hukuwa na hufa. Mwana falsafa wa kiothomani Katip Çelebi naye pia alikuwa na falsafa iliyofanana nay a Ibni Haldun. Kiuhalisia tunaona tamaduni na mataifa yaliyokuwa makubwa katika historia muda ulivyopita tamaduni na mataifa hayo yalififia. Kama inavyosemwa kitu pekee kisichobadilika katika maisha ni mabadiliko yenyewe.

 

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL  mkuu wa kitivo cha siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anatufafanulia kuhusiana na mada hii..

                    Katika dunia yetu ya leo pia inajiri michakato inayoshabihiana. Marekani inaonekana haipo katika hali ya kuongoza katika ushindani wa kiulimwengu wa kuichumi, kiteknolojia, kisiasa na kimisingi (uadilifu, haki za binadamu na misimamo ya kimaadili). Wala haitegemewi kurudi katika hali ya kuongoza katika ushindani wa kilimwengu katika nyanja hizo. Ni kwa ajili hiyo ili iweze kubakia kuwa kiongozi wa kidunia imekuwa ikizidi kutumia sera ambazo zipo kinyume na utandawazi na za ubinafsi, vikwazo vya kiuchumi na vita, na yapaswa kufahamika aina hii ya siasa itabidi iendelee kutumiwa na taifa hilo. Aina hii ya siasa ya kujihami ina matokeo mabaya sana lakini historia inatuambia kwamba bado  hayajatokea mataifa yenye siasa zinazojenga na kuleta utulivu yatakayoongoza katika ushindani wa kidunia.

                      Tunaona kadiri siku zinavyokwenda siasa za kimifarakano, za kiuvamizi wa kiuchumi na kijeshi za Marekani dhidi ya mataifa kama China, mataifa ya magharibi, Amerika ya kusini, Uturuki  na hivi karibuni Iran zikizidi kuongezeka. Marekani kujitoa peke yake katika mkataba wa kinyuklia, kurudisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran, kupanda tena kwa joto katika mlango bahari wa Hormuz , maelezo makali ya kila mmoja kwa mwenzie ni katika viashiria hai vya  mvutano ulioongezeka.                 

                    Marekani mara zote imekuwa ikiionya na kuitishia Iran ili isitengeneze silaha za kinyuklia. Ndiyo bila shaka yeyote ni suala lisilo kubalika kumiliki silaha ambazo ikitokea zikitumika zitaangamiza sio tu wanadamu bali na viuembe hai wote, kama ilivyofanya Marekani kwa Japan. Pamoja na hayo kama vile Israel, India, Marekani na mataifa mengine yanavyopata hofu Iran kumiliki silaha hizo, vivyo hivyo Iran nayo inapata hofu kwa mataifa hayo kuwa na silaha hizo za kinyuklia.Kitendo cha kuona katika ukanda na hasa Israel inamiliki na kutumia silaha za kikemikali kinaihalalishia Iran nayo kujaribu kujimilikisha silaha hizo, kwani kitendo cha kuizuia kinaonyesha wazi hakizingatii misingi ya uadilifu

Kujitanua kwa Iran

                           Katika ukanda tunaiona Iran imeachwa peke yake ikikabiliana na vitisho vya Marekani. Na sababu kubwa ya hili ni siasa za kujitanua za Iran zinazozingatia madhehebu. Inaweza kusemwa Iran ipo katika hali ya kujitenga kabisa kwani ipo mbali na udhibiti wa mji mkuu wa nchi nne (Irak, Yemen, Syria na Lebanon).

İran pamoja na mataifa ya kibeberu zinatumia njia ambazo zinashabihiana kwa kiasi kikubwa. Nchi hizi zote zimekuwa zikiingilia siasa maeneo ambayo yapo karibu nayo.

Sera za Iran za kimadhehebu zimeleta shida katika ukanda kuliko hata zile za Israel. Sababu moja kubwa ya nchi za ghuba kuangukia katika siasa za kimwelekeo wa Israel ni siasa za kujitanua na za kiuvamizi za Iran. Je ni kwa kiasi gani Iran inaleta madhara kwa Israel ?  ina madhara yeyote ? ni masuala ya malumbano. Lakini siasa hizi za Iran ni moja ya sababu kubwa ya kutokuwepo kwa utulivu katika mataifa ya kiislamu.

 

Uvamizi wa Marekani

                               İran, inaweza kupingwa kwa mambo mengi yakiwemo yaliyotajwa hapo juu na ambayo haykutajwa. Lakini pamoja na utofauti huo wa Iran unaopingwa haitoi uhalali na haki kwa Marekani kufanya uvamizi dhidi ya siasa za Iran. Kwa sababu Marekani haitazami kwa mtazamo wa uadilifu. Sera za Marekani kwa Iran zimejengwa kutokana na kuzingatia maslahi yake ya kibeberu. Fasili ambayo ipo tangu karne ya 19 na 20. Sera za kilimwengu za Marekani chini ya uongozi wa Trump, zinashabihiana sana na sheria za mkuu wa polisi wa kijiji dhidi ya wahindi wekundu.

Kwa upande mwingine inafahamika kwamba hakuna nchi yeyote iliyokaliwa kimabavu na Marekni au mataifa ya magharibi ilipata furaha na amani. Aina hizi za uvamizi katika eneo zimesababisha mamilioni ya vifo, damu, machozi, ukimbizi mazingira ya kukosekana kwa uadilifu na kutotenda haki yaliyosababisha makundi ya kigaidi kuundwa kiurahisi zaidi..

Kinachoweza  za kutokea kutokana na uvamizi huu..

              Inawezekana Marekani inataka kuilazimisha Iran kukubali masharti kwa kuukuza mvutano na kuzidisha vikwazo. Mvutano huu unaweza usibadilike na kuwa vita kama ilivyotokea mara nyingi huko nyuma. Tunatumaini mvutano huu  kwa namna yeyote ile hautaishia kuwa vita ya kisilaha. Lakini katika dunia ambayo kupoteza uchaguzi kunaonekana ni kubaya zaidi ya kupoteza vita. Inatubidi kutegemea uwezekano wa kuibuka kwa vita.

Baada ya nchi zingine Iran nayo itaondolewa utulivu, itageuzwa kuwa Syria, Mashariki ya kati ya namna hii haiwezi kuwa sawa na ilivyokuwa mwanzo. Utulivu wa mwisho uliobaki mashariki ya kati, pamoja na amani ya moyo vinaondolewa. Kama ilivyokuwa baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia, nchi za kibeberu zinalifanya eneo la mashariki ya kati kuwa uwanja wa mbio za farasi. Hali hio itasababisha athari hasi zaidi kwa  Uturuki kuliko hata masuala ya Syria.

Katika mashariki ya kati ambayo mataifa yote yameparaganyika huku nchi za ghuba zikiwa na uongozi wa vibaraka inamaanisha kwamba mipango mikuu ya Israel haitakuwa na vikwazo wala mpinzani.

Uvamizi wa Marekani Iran kama ilivyokuwa kwa masuala ya Syria, inakuwa ndio mshindi pekee katika mashariki ya kati, hata kama siyo Marekani yenyewa basi Israel. Nchi za ghuba ambazo zinaonyesha kuwa pamoja na hata kuonyesha kuishawishi Marekani dhidi ya vitisho vya Iran, bila shaka nazo hazitakuwa salama wala hazitaachwa huru pindipo vitisho vya Iran vitakapomalizwa. Endapo nchi hizi zitaendelea kubaki kama nchi basi  Marekani na Israel zitaendelea kuzitawala  nchi hizi zaidi na zaidi.

 

Uturuki ifanyaje ?

                                      Uturuki inafahamu migogoro ya kikanda isipotatuliwa na wadau wa dunia, husababisha hali kutoweka kwa utulivu, huleta hali ya kuongezeka kwa chuki na kusababisha vitendo vya kigaidi kushamiri. Kutokana na hayo pamoja na msimamo wake wa kiadilifu Uturuki imekuwa ikifuata siasa zinazozingatia kanuni, misimamo yake kwa Syria. Iran, Irak na nchi nyingine ni mfano wa wazi.

Pamoja na kuendeleza misimamo yake inayozingatia kanuni, Uturuki inaweza kutumia njia zote za kidiplomasia kwa kufanya majadiliano ya kina na Umoja wa Ulaya, China, Urusi, nchi za ghuba na hata Marekani na Iran ili kuzuia mapigano ya kivita  yanayoweza kutokea na kuwezesha mchakato huu uratibiwe kwa njia za amani.

                                  Huko nyuma  Uturuki iliweza kuweka misingi iliyopelekea Iran na Brazil kufikia makubaliano.Makubaliano yake na Urusi yamezuia mamilioni ya wasyria kuangukia katika ukimbizi. Uturuki imekuwa ni mchangiaji mkubwa wa amani duniani kuanzia bara hindi had Balkani, toka Afrika hadi Afghanistan. Kwa vile nchi zenye misimamo ya kikanuni yanapokuja masuala ya kidunia zimebaki chache,  na kwa vile  Uturuki ndio rais  wa Ushirikiano wa nchi za kiislamu basi ni budi ifanye kila linalowezekana kuzuia mvutano wa Iran na Marekani kugeuka kuwa vita.

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt.Habari Zinazohusiana