Mvua kubwa na radi vyasababisha vifo vya watu 22 Iran

Kutokana na dhoruba na mvua kubwa watu 22 wamepoteza maisha katika maeneo tofauti  nchini Iran.

Mvua kubwa na radi vyasababisha vifo vya watu 22 Iran

Kutokana na dhoruba na mvua kubwa watu 22 wamepoteza maisha katika maeneo tofauti  nchini Iran.

Msemaji wa masuala ya dharura ya Iran Mücteba Khalidi, katika taarifa yake ya maandishi, ameorodhesha maeneo yaliyoathiriwa na mvua hiyo kali ukiwemo mji wa Ardabil, Azerbaijan Mashariki, Azerbaijan Magharibi, Zanjan, Rezevi Khorasan,Khorasan Kusini, Çaharmahal-Bakhtiari, Isfahan, Kermanshah, Fars, Khuzestan, Kerman, Lorestan.

Mvua hiyo imeripotiwa kuanza tangu 8 Mei na kusababisha vifo vya watu 22 nhuku watu wengine 53 wakiwa wamejeruhiwa.

Kulingana na Khalidi, kati ya watu 22 waliopoteza maisha wawili walimezwa na maji huku wengine 20 wakiwa wamepigwa na radi.

Katika mvua zilizoanza tarehe 17 Machi na kuchukua mwezi mzima watu 78 waliripotiwa kufariki huu wengine elfu moja wakiwa wamejeruhiwa nchini humo.

 


Tagi: mvua , vifo , Iran

Habari Zinazohusiana