Matamshi ya mauaji  ya kimbari  ya Trump hayawezi kuidhuru Iran

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Jawad Zarif ajibu matamshi ya mauaji ya kimbari ya rais wa Marekani kuhusu Iran

Matamshi ya mauaji  ya kimbari  ya Trump hayawezi kuidhuru Iran

Zawad Zarif, waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema kuwa matamshi ya mauaji ya kimbari yaliotolewa na rais wa Marekani Donald Trump  hayana uwezo wa aina yeyote ile  kuirejesha nyuma Iran.

Zarif amesema kuwa kauli za mauaji ya halaiki ya Trump  dhidi ya Iran na ugaidi wa kiuchumi  havitoweza kulidhuru taifa kongwe la Iran.

Rais wa Marekani ilipeperusha ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter akifahmisha kuwa iwapo Iran itataraji kupigana vita ba Marekani basi ndio itakuwa mwisho wake.

Katika ujumbe wake wa kumjibu Trump , waziri wa mambo ya nje wa Iran Jawad Zarif amekumusha kuwa mfalme Alexanda the Great, Cenghiz Khan na viongozi wengine zaidi ya Trump walijaribu kuidhuru Iran bila ya mafaanikio kwa kipindi cha miaka zaidi ya 1000, matamshi ya Trump hayana athari yeyote kwa Iran.

Usijaribu kumtisha raia wa Iran, muheshimu na uzungumze nae alisema  pia Jawad Zarif katika ujumbe wake huo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema kuwa Marekani inatumwa na B Team aliwa na maana mshauri wa ikulu ya White House John Bolton, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, mwanamfalme wa Saudia Bin Slaman na mwanamfalme wa Abu Dhabi Mohammed bin Zyed.

Hali ya vuta ni kuvute kati ya Iran na Marekani imeongezeka  tangu Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia na Iran mwaka 2015 na kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran.

Marekani imetuma mashua yake ya kivita USS Abraham Lincoln na ndege za kivita B-52 Mashariki ya Kati.Habari Zinazohusiana