Zaidi ya waumini laki 2 waswali swala ya Ijumaa msikiti wa Al Aqsa

Zaidi ya waumini laki 2 wengi wao wakiwamo wapalestina wamiminika msikiti mtukufu wa Al Aksa kuswali swala ya Ijumaa

Zaidi ya waumini laki 2 waswali swala ya Ijumaa msikiti wa Al Aqsa

Katika ijumaa ya pili ya mwezi mtukufu wa Ramadhan,Wapalestina wamiminika kwenda kuswali swala ya Ijumaa katika msikiti mtukufu wa Al Aqsa, pamoja na ugumu na mapingamizi yote yaliyowekwa na Israel.

Kuanzia mida ya asubuhi makumi kwa maelfu ya Wapalestina wamekuwa wakipita vituo mbalimbali vya kukaguliwa vilivyopo kati ya eneo liliyokaliwa kimabavu la ukanda wa gaza na Jerusalem.

Kwa mujibu wa Uongozi wa taasisi ya waislamu wa Jerusalem, zaidi ya watu laki 2 wameswali swala ya ijumaa katika msikiti mtukufu wa Aqsa.

Kwa upande mwingine vyanzo vya habari vya eneo hilo vimeripoti kwamba Israel imezuia watu 200 waliojitolea kwa ajili ya kutoa huduma kwa waumini wanaofika kufanya ibada katika msikiti huo.

Katika khotuba ya Khatibu wa Ijumaa wa msikiti wa Al Akqa, Sheikh Ismail Nawahde aliusia ulimwengu wa kiislamu na kiarabu kuutetea msikiti huo mtukufu wa Al Aqsa.

Kuanzia mwaka 1967 Israel inakalia kimabavu eno la mashariki mwa Jerusalem na Ukanda wa Gaza.Habari Zinazohusiana