Uzoefu wa Uturuki: Njia ya Khorasan

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt

Uzoefu wa Uturuki: Njia ya Khorasan

    Kwa mtu anayeyatizama maisha kwa mtazamo chanya, kuandika mambo yaliyo hasi sio kitu rahisi. Ningependa kuwaletea upembuzi kuhusu dunia inayoelekea kwenye amani na furaha, ambayo inaimba zaidi nyimbo za uhuru, na inayoleta habari njema za undugu na sio habari za mapigano.

 

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anafafanua kuhusiana na mada hii...

 

Kwa bahati mbaya Marekani, Urusi,China na wadau wengine wakuu kila uchwao wanatusogeza zaidi katika dunia yenye mafarakano. Pamoja na wadau wa kidunia, ugaidi unaofanywa na mtu mmoja mmoja  au ule unaofanywa na makundi kila uchwao unafanya sehemu salama kwa ajili ya maisha ya familia kuwa finyu. Kadri siku zinavyozidi kwenda mataifa ya magharibi yanajongelea hali ya mashaka kama ilivyokuwa kabla ya vita kuu ya 2 ya dunia. Mashambulizi angamizi dhidi ya watu mbalimbali, akili za kinyama kama inavyofanywa na DAESH, ilivyofanyika New Zealand na Sri Lanka. Kadiri tunavyokumbuka Utaranti na Uvanjelisti tunaona ni jinsi gani dunia ilivyo katika giza.

Iwe katika dunia ya kiislamu au Ulimwengu mzima kwa ujumla tunahitaji lugha ya pamoja dhidi ya matukio haya yanayoiweka dunia gizani siku hadi siku. Kuna haja ya kila mmoja kuwa na maadili ya kiujumla yanayo alika  watu wote kuishi na kuzitii tabia fulani.

Kuanzia na maeneo mengine na haswa katika eneo la dini,  pale ambapo dini zinapounganika na kwa umoja wao wakafuata dini zao kiundani Je hilo halitatua matatizo yaliyo mengi ya familia ya mwanamdamu ?

Binadamu humpenda zaidi mtu anayefanana naye. Je ni kwa nini hilo linapofanyika kunakuja kutenga, kubagua na kufanya uadui ?

Badala ya tofauti kuonekana kama ni vitisho, inapaswa zionekane kama fursa, utajiri na inapaswa zikaribiwe kwa uvumilivu, tofauti na amani na furaha ni kitu gani kitapatikana ?

 

            

Je msingi wa furaha na utulivu sio kwamba ni zaidi ya kupokea bali kufikiria na kutekeleza kutoa na kutumia pamoja?

              Ili kuweza kuishi pamoja, Je sio suala la kuzingatia, kutowashusa walio tofauti na kutoona kwamba dini, rangi, asili, lugha, ideolojia,kabila au jinsia ni vyanzo vya ubora.?  

Kimsingi nyingi ya tabia tulizozitaja hapo juu ni tabia ambazo hivi sasa zinajulikana kama tabia za kiujumla. Lakini kama tulivyokwisha kusema katika moja ya makala zilizopita kwamba hivi sasa tunaishi katika kipindi ambacho tunaweza kukiita ni zama za mwisho wa maadili. Zamani ni baadhi tu ya maadili ndiyo yalikuwa yakivunjwa, Lakini hivi sasa tunaishi katika kpindi ambacho maadili yote yanavunjwa. Kwa upande mwingine tuna maadili mengi ambayo yanakubalika kinadhiria yapo katika makaratasi lakini hayatekelezwi kivitendo.

Leo hii tumefikia hatua ambayo  mifarakano zaidi, siasa kali, ubaguzi, ukandamizaji na mambo mengine kama hayo yote yapo duniani.

Je hakuna kiipindi katika historia maadili tuliyoyataja hapo juu yalitekelezwa kivitendo na sio kuwako tu kinadharia ?

Kwa mtazamo wa ustaarabu wetu kiwepesi kabisa tunaweza kusema kwamba jawabu la swali hilo ni ndio.

Kimsingi utambuzi, uelewa, ufafanuzi kutoka eneo la Khorasan kwenda dunia nzima ulikuwa ni chanzo cha maadili tuliyoyataja na ambayo hatukuyataja hapo juu kukubalika na kutumika.

Njia hii/ Shule hii inafahamika kwa majina mengi kama vile njia ya Khorasan, Yesevi, Usufi, Watakatifu wa Khorasan, Mevlevi na mengineyo. Vyovyote itakavyoitwa yaliyomo katika njia hiyo ni yale yale. Mimi nimeamua kuchagua jina la Njia ya Khorasan kwa kuwa inaelezea fikra na harakati za binadamu zilizoanzia eneo la kijiografia la Khorasan na kuenea ulimwengu mzima.

Kwanza kabisa tuelezee Khorasan inapatikana wapi. Ni eneo la kihistoria  ambalo lilijumuisha İran, Afganistan, Tacikistan,Türkmenistan, Kırgızistan, Kazakistan, na baadi  ya miji ya  Uzebakistani kama vile Merv, Herat, Nişabur, Belh, Buhara, Semerkant. Tukianza na Hoca Ahmet Yesevi kisha Şahı Nakşibendi, Mevlana Celaleddin Rumi, Hacı Bayramı Veli, Hacı Bektaşı Veli ni katika majina maarufu na yenye heshima kubwa kutokea eneo hili la Horasan ambao jumbe zao zilienea dunia nzima. Ahi Evran, Yunus Emre, Sarı Saltuk, Somuncu Baba, Gül Baba nao pia katika majina yanayofahamika yaliyoiendeleza njia hio.

                        Sifa kubwa ya msingi ya wenye majina haya ni kwamba walipokuwa wakieneza jumbe za kiujumla kutoka katika tamaduni za kiislamu hawakubagua, hawakutenga hawakujiona ni bora kuliko walio tofauti na wao waliunganisha dini/tamaduni/ na umoja wa kijamii walikuwa ni watu wavumilivu.Hii leo  maadili hayo ambayo yanafahamika kama maadili ya kiujumla kuyachukua tu haitoshi bali kuyaishi na kuyafanya kuwa ndio mtindo wa maisha na msimamo wa kitabia. Ni kwa ajili hiyo wakati katika mataifa ya magharibi watu wenye imani tofauti walisakamwa na kuhojiwa, katika jiografia ya dola la Othoman wenye majina hayo ambao walikuwa ni kama kurunzi baharini walitumia nguvu zao kuelimisha na kuhabarisha na hatimae kuwawezesha wasiokuwa waislamu kuweza kuishi katika dola hilo ambalo wengi wa wakaazi wake walikuwa ni waislamu, wakidumisha imani zao. Leo pamoja na maadili ya kiujumla kupeperushwa kama bendera. Katika maeneo mengi hatuoni mtazamo huo uliowekwa na njia ya Khorasan.

Misingi mikuu ya njıa ya Horasan inaelezewa vizuri kupitia ubeti huu wa Mevlana:

Katika ukarimu na kutoa msaada  kuwa kama vile maji yanayotiririka.

Katika huruma na upendo kuwa kama  jua.

Katika kutunza siri za watu wengine kuwa kama  usiku.

Katika hasira na hamaki kuwa kama  mfu.

Katika unyenyekevu na uwoga kuwa kama  udongo.

Katika uvumilivu kuwa kama  bahari.

Onekana kama ulivyo, au kuwa kama unavyoonekana.

Maneno ya swahaba wa mtume Ali “Watu nı wenzako katıka kuumbwa au nı nduguzo katıka dını” ndiyo yalikuwa falsafa ya msingi ya njia ya Horosan

Njia hii, mtazamo huu, udhoefu huu ulionzia Khorasan na kisha kuenea dunia nzima kimsingi tunaweza kuuita udhoefu wa kituruki.

Kwa minajili hiyo basi inawezekana udhoefu wa kituruki ni moja ya suluhisho la kipekee dhidi kujifungia, kujitenga, ubaguzi kwa waislamu na watu wote kwa ujumla.Njia za kilimwengu ambazo zinasifu yale yaliyokuwa na maslahi kwazo, huku ikikemea mengine yote yasiokuwa na faida kwayo. Njia ambazo hazina mizizi wala hazifuati utamaduni, zinaweza kuwa suluhisho kwa muda mfupi lakini kwa muda wa kati na muda mrefu uwokovu wa mwanadamu utategemea njia yenye misingi yake katika utamaduni zinazotokana na vitendo kihistoria zinazozingatia tabia njema ambayo unaweza kuiita kama njia ya Khorasan

 

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım BeyazıtHabari Zinazohusiana