Ndege yaanguka uwanja wa kimataifa wa Dubai

Ndege ndogo yaanguka katika uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Ndege yaanguka uwanja wa kimataifa wa Dubai

Ndege ndogo yaanguka jijini Dubai moja ya miji inayopatikana Falme za kiarabu (UAE). Watu wanne wamefariki kutokana na ajali hiyo. Miongoni mwao ni raia 3 wa Uingereza , na raia 1 wa Afrika kusini.

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na WAM, shirika rasmi la habari la   Umoja wa Falme za kiarabu, ndege ndogo iliyosajiliwa nchini uingereza aina ya  Diamond DA42 imeanguka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai.

Safari katika uwanja huo zilirejeshwa katika hali ya kawaida baada ya kucheleweshwa kwa muda mfupi.

Ofisi ya habari ya serikali ya Dubai imefahamisha kwamba ndege hiyo kuna uwezekano imeanguka kutokana na tatizo la kiufundi.


Tagi: UAE , Dubai , Ndege

Habari Zinazohusiana