Ziara ya waziri wa Iraq nchini Uturuki

Waziri Mkuu wa Iraq Adil Abdulmehdi amefanya ziara nchini Uturuki baada ya kupewa mwaliko rasmi na rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdoğan.

Ziara  ya waziri wa Iraq nchini Uturuki

Waziri Mkuu wa Iraq Adil Abdulmehdi amefanya ziara nchini Uturuki baada ya kupewa mwaliko rasmi na rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdoğan.

Kwa mujibu wa habari Adil Abdulmehdi amepokelewa na Erdoğan katika hafla maalumu Beştepe mjini Ankara.

Baada ya hapo viongozi hao wamefanya mkutano wa faragha na kisha kuzungumza na ujumbe wao.

Viongozi hao wawili wamezungumia mapambano dhidi ya ugaidi,ujenzi wa Iraq,ushirikiano wa kibiashara kati ya Iraq na Uturuki hasa katika kitengo cha nishati.

Mahusiano ya kikanda na kimataifa ni kati ya mada zilizojadiliwa pia kati ya Erdoğan na Adil Abdumehd.Habari Zinazohusiana