Taasisi ya YTB yafanya ziara Kaskazini mwa Syria

Uongozi wa taasisi inayohusika na udhamini wa masomo nchini Uturuki YTB yafanya zaira Kaskazini mwa Syria

Taasisi ya YTB yafanya ziara Kaskazini mwa Syria

Uongozi wa taasisi  ya waturuki waishio ugenini  na udhamini wa masomo YTB  imefanya ziara Kaskazini mwa Syria.

Ziara hiyo imefanyika katika ameno ambayo jeshi la Uturuki liliendesha operesheni ya Tawi la Mzaituni na operesheni ya Fratia.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo Abdullah Eren  ameongoza tume iliaoshirikiana nayo katika ziara hiyo.

Tume hiyo imetembelea   chuo kikuu cha Azez, Jarabkuz, Bab ba Çabanbey Kilis.

Abdullah Eren ametembelea pia  raia na watoto  yatima  ambao alichangia nao mlo wa jioni katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Yatima hao wanapatikana katika kituo cha kulea yatima cha Musa Özalkan ambae alikuwa shujaa wa kwanza  wakati kulipoanzishwa operesheni ya Afrin.

Katika juhudi za kuwarejesha wanafunzi waliosimamisha masomo yao kutoka na vita, uongozi wa YTB  umefahamsha kuwa utaendelea na tafiti zake ili kuwapo fursa wanafunzi hao kuendelea na masomo yao na kuwa dhamana kubwa ya kuijenga Syria baada ya vita.

Mkurugenzi Abdullah Eren amesema kuwa wanafunzi hao  watapewa fursa ya kuendelea na masomo yao  na kuondoa moja kwa moja vitisho vya ugaidi.Habari Zinazohusiana