Utaranti wa Sri Lanka

Ufafabuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kkitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt

Utaranti wa Sri Lanka

Tumeanza wiki na shambulizi la kigaidi. Safari hii shambulizi la kigaidi limefanyika, Sri Lanka,  nchi jirani ya India inayopatikana mashariki mwa bara la Asia. Katika mji mkuu Colombo na miji mingine mitatu yamefanyika mashambulizi saba katika makanisa matatu na Hoteli nne wakati wakristo wakiwa wanasheherekea sikukuu ya pasaka. Mpaka hivi sasa watu 300 wamepoteza maisha na zaidi ya watu 500 wamejeruhiwa.

    Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL  mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anafafanua...

Sri Lanka  na mapigano ya ndani

Kutokana na mashambulizi hayo jamii ya Wasri Lanka wapo katika hali ya hamaki na hudhuni kubwa. Ni kwa sababu hiyo ni siku za kuonyesha mshikamano na wa Sri Lanka.

Katika mashambulizi hayo mpaka hivi sasa raia wa kigeni 36 wamepoteza maisha.Miongoni mwao wakiwemo waturuki na waislamu. Kati ya raia wa kigeni waliopoteza maisha wapo pia wamerekani, waingereza, wahindi na wadenmark.

Baada ya mashambulizi hayo serikali ilipiga marufuku raia kutembea nje . Mitandao yote ya kijamii ilifungwa.

Sri Lanka ni kisiwa ambacho kina wakaazi wanao karibia milioni 22. %70 ya wakaazi wa nchi hio ni waumini wa dini ya kibudha %12 ni waumini wa dini ya kihindu %9 ni waumini wa dini ya kiislamu na %6 waumini wa dini ya kikristo wa dhehebu la katoliki .

Kati ya mwaka  1983-2009 nchini Sri Lanka kulikuwa na vita vya ndani baina ya  wasinha wa kibudha na watamili wa kihindu.Vita hivi vya wenyewe kwa wenyewe vilimalizwa na majeshi ya serikali mnamo mwaka 2009. Mpaka hivi sasa hakuna aliyejinasibu kutekeleza shambulizi hilo hali kadhalika sababu za shambulizi hilo hazijafahamika. Mpaka hivi sasa hakuna kundi la kigaidi linalofahamika nchini humo kwa kufanya matukio ya kutisha  kama hayo.

Katika vipindi tofauti nchini Sri Lanka kumekuwa na mashambulizi yanayofanywa na waumini wa kibudha dhidi ya wakristo na waislamu. Siku za hivi karibuni imefahamika kwamba makanisa yameshambuliwa mara 26 na waumini wa kibudha. Katika shambulzi la mwaka 2013 lililotekelezwa na waumini wa kibudha waumini 40 wa dini ya kiislamu waliuawa.

Muitikio wa dunia

Hata wale viongozi  ambao hawakusema chochote katika shambulizi la kigaidi dhidi ya misikiti nchini New Zealand,safari hii wamepaza sauti zao kulaani mashambulizi hayo. Wamefanya kama inavyohitajika kufanywa katika nyakati kama hizi. Tunatumaini aina hii ya tabia itafanyika katika kila tukio la kigaidi na kutakuwa na ushirikiano zaidi.

Rais wa Uturuki Recep Tayyib Erdoğan naye amelaani vikali shambulizi hilo la kigaidi. Katika maelezo ya Erdoğan alisemba shambulizi hili ni shambulizi dhidi ya Utu na akatolea wito ushirikiano wa kidunia katika vita vya kutokomeza ugaidi: alisema rais “Nalaani vikali shambulizi la kigaidi lililofanyika nchini Sri Lanka katika maadhimisho ya pasaka. Shambulizi limefanywa dhidi ya Utu.Ni shambulizi la kinyama ni mara nyingine tena inajidhihirisha kwamba vita dhidi ya ugaidi wa aina yeyote ile ni suala la msingi sana. Tushikamane pamoja na Sri Lanka katika kupiga vita ugaidi ambao ni adui wa amani na Utu”

Srilanka na Utaranti “Tarrantizmi”

Mashambulizi dhidi ya waislamu wasio na hatia waliokuwa wakifanya ibada misikitini nchini New Zealand na hivi sasa mwezi mmoja na nusu baadae mashambulizi dhidi ya wakristo wasio na hatia walikuwa katika ibada ni masuala yanayoshitua. Kama vile nilivyoandika katika makala zilizopita baada ya mauaji ya New Zealand kwamba aina hii ya ugaidi ambayo inatokana na ubaguzi uliojidhihirisha kwenye waraka “manifesto” aliousambaza mtekelezaji wa mauaji yale, Brenton Tarrant, ubaguzi uliozingatia kwamba wazungu wa Ulaya ndio watu bora kuliko watu wengine wote niliufafanua kama Utaranti “Tarantism”.Kama vile ubaguzi wa kiserikali ulivyopewa jina la Ufashisti au ubaguzi wa kitaifa ulivyopewa jina la Unazi au ule wa kidini ulivyopewa jina la “Siyonizm”, tuliona kuna kila sababu ya kuupa jina ubaguzi huu wa rangi unaozingatia kwamba wazungu wa Ulaya ndio watu bora.

Na kwa madhalimu waliotekeleza mashambulizi ya Sri Lanka bila kuzingatia sababu zilizowapelekea kufanya walioyafanya, wala nani alietekeleza wanapaswa kutafutwa na kupewa adhabu kali sana, na aina hii ya ugaidi inapaswa kulaaniwa. Kimsingi watekelezaji wa matukio haya fikra zao hazitofautiani na za Tarrant.

Wito wa haki

Katika zama zetu matukio mbali mbali ya kigaidi yamekuwa yakitekelezwa na watu kwa kisingizio cha Uislamu, ukristo, ubudha, usekulari au kwa dini na ideolojia nyingine.Bila shaka yeyote hakuna sababu yeyote inayoweza kuhalalisha. Pamoja na hayo tunapaswa kuona kwamba vitendo vya kigaidi vinaongezeka kadri hali ya mbinyo wa haki unavyoongezeka. Bila shaka hata kama haki itapatikana  bado baadhi ya watu wataendelea kufanya vitendo vya kigaidi. Lakini kwa kiasi kikubwa ugaidi utakuwa umepunguzwa. Kwa hiyo tunaweza kusema kwamba dawa ya kuzuia ugaidi ni kutenda haki. Tunachotakiwa kufanya ni kujenga mifumo ya kutenda haki ambayo itawazuia watu kuangukia katika siasa kali. Maneno ya Oliver Roy kwamba “ Uislamu hauwezi kuwa siasa kali, Siasa kali zinaweza kufanywa ni uislamu”  yanaelezea sababu za mashambulizi mengi ya kigaidi. Kadiri watu wanapokuwa wafuasi wa siasa kali ndivyo wanavyojaribu kuweka uhalali wa vitendo vya kigaidi katika dini zao na idiolojia zao. Wito wetu kwa ngazi ya kidunia juu ya haki ni kwa ajili ya kukausha chanzo cha vitendo vya kigaidi.Ni lazima kuzuia fikra  za siasa kali zinazopelekea kuzaa vitendo vya kigaidi. Katika juhudi za kuleta haki kidunia inabidi siasa kali zisifanywe kuwa ni Ukristo, Uislamu, Ubudha au Uyahudi. Kama hatutafanya jitihada za kutafuta haki kidunia, tukaishia kufanya jitihada za kutafuta haki kwenye mataifa yetu tu basi dunia itaendelea kuwa si salama kila uchwao. Kwa sababu katika zama hizi za sayansi na teknolojia ukosefu wa uadilifu, dhulma na kutotenda haki vinaonekana haraka zaidi na kwa uraisi zaidi. Kwani uwezo wa binadamu kuficha dhulma hizo unapungua kwa kasi katika zama hizi.

Mashambulizi ya Septemba 11, Mashambulizi ya ISIS, Mahambulizi ya Ankara, Paris na London, mashambulizi ya Tarrant dhidi ya misikiti New Zealand, na haya mashambulizi ya mwisho dhidi ya makanisa Sri Lanka yote yanaonyesha kwamba jamii ya binadamu kila mahali inakabiliwa na janga kubwa la ugaidi. Kokote kule tutakapoishi, hatari ya mashambulizi haya inaongezeka kila uchwao na kuyaweka maisha yetu  hatarini. Ni kwa sababu hio kadiri tunavyoongeza juhudi za kuleta uadilifu na kutafuta haki kwa upande mmoja kwa upande mwingine ugaidi utakaofanywa bila kuzingatia makusudi yake, binadamu wote wanapaswa kuulaani.Kwa upande mwingine kuyadharau baadhi ya matukio ya kigaidi na kuyaacha yapite ni kuzidi kuyaweka maisha yetu hatarini.

Imefafanuliwa na Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kkitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım BeyazıtHabari Zinazohusiana